Familia ya
mgonjwa wa kwanza wa Ebola aliefia nchini Marekani imelalamika kwamba
kama ndugu yao angepewa uangalizi na matibabu kama inavyotakiwa basi
asingepoteza uhai wake.
Thomas Duncan alietokea Afrika Magharibi zaidi ya siku 18 zilizopita
ambapo mchumba wake aitwae Louise Troh waliekua waoane baada ya Duncan
kuwasili Marekani, ni mmoja wa watu wa karibu waliolalamikia huduma
mbovu na ‘kubaguliwa’ kwa Duncan baada ya kugundulika kuwa mgonjwa wa
Ebola hivyo anataka uchunguzi ufanywe.
Anasema Duncan alipotua Texas kwa mara ya kwanza aliambiwa aende
nyumbani na wala hakupimwa kama anavyo virusi vya ugonjwa wa Ebola
pamoja na kwamba aliwaambia Manesi kwamba ametokea Liberia ambako kuna
Ebola.
Reverend Jesse Jackson akiwa na mama mzazi wa Duncan.
Ndugu mwingine wa kiume wa Duncan amesema mgonjwa wao hakuwa chini ya
uangalizi mzuri kama ilivyotakiwa na alibaguliwa kwa sababu ya weusi
wake, yani kuna wale Wagonjwa wazungu waliokutwa na Ebola waliwekewa
uangalizi mzuri mpaka wakapona ila huyu sababu ni mweusi akatelekezwa.
Hii picha ni Duncan akiwa na ndugu yake muda mfupi baada ya kuwasili Marekani kwenda kumuoa mchumba wake wa siku nyingi.
Louise Troh mchumba wa Marehemu Duncan anaeonekana upande wa kulia.
Duncan aliekua na umri wa miaka 42 muda mfupi kabla ya kufariki
alikua akitaka kumuona mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 19
anaeonekana kwenye picha hapa chini lakini haikuwezekana.
Hawa kwenye picha hapa chini ni watu waliobobea kwenye usafishaji na
waliitwa kufanya usafi kwenye nyumba aliyokua anakaa Duncan huko Dallas
Texas kabla ya kwenda Hospitali ambapo vitu vyake kama mashuka na
mataulo vilibaki kwenye nyumba hiyo kwa siku tano baada ya yeye
kupelekwa Hospitali.
0 comments:
Post a Comment