Wednesday, October 15, 2014

MAMBO 10 MUHIMU UNAYOPASWA KUMFANYIA MWANAMKE UMPENDAYE AWE NA FURAHA ZAIDI

1. Mpigie simu hata mara 1 kwa siku kumjulia hali. ukibanwa sana, jaribu kumtumia hata ujumbe mfupi kuonyesha unamjali.
2. Msikilize kwa makini wakati aongeapo.
3. Chunguza kwa makini vitu anavyopenda na asivyopenda.
4. Msifie/mpongeze vizuri na kwa dhati mara nyingi iwezekanavyo.
5. Mnunulie kadi ama maua, wakati mwingine.sio lazima vya bei mbaya.
6. Mpeleke kwa chakula cha jioni. sio lazima iwe hotel ya nyota 5 kila siku. sehemu yeyote nzuri itafaa.
7. Kuwa na upendo, sio fujo. mahitaji yake daima yaje kabla ya kwako.
8. Fanya mambo upendayo (kutazama soka, kuogelea n.k), pia fanya baadhi ya vitu apendavyo kufanya yeye (kutazama filamu, kwenda kununua         mahitaji inapotokea n.k) ili furaha yenu ikutane.
9. Mnunulie vitu vyenye maana na atakavyofurahia. sio lazima iwe iphone 6, hata shuka zuri litamfaa pia.
10. Onana naye mara kwa mara kadri iwezekanavyo.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI