Mama wa marehemu, Steven Kanumba, Flora Mtegoa (mwenye kipaza sauti) akizungumza jambo.Mayasa Mariwata
MAMA wa marehemu, Steven Kanumba, Flora Mtegoa amekanusha vilivyo taarifa zilizozagaa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na kijana mdogo ambaye amemzidi umri (serengeti boy).
Mama
Kanumba ambaye pia amefuata nyayo za mwanaye kwa kujiingiza katika
uigizaji, alifunguka hayo alipokuwa akizungumza na mwanahabari wetu
mambo mbalimbali yahusuyo maisha yake binafsi na sanaa kwa jumla.
Lilipofika
suala la tuhuma hizo ambazo zimewahi kuripotiwa na baadhi ya magazeti
(si ya Globa Publishers Ltd) kwamba anatembea na dogodogo, mzazi huyo
alisema taarifa hizo ni za kipuuzi na hazina ukweli wowote.
“Huo ni
uongo tu kwa kweli, hakuna kitu kama hicho, mtu mzima kama mimi naanzaje
kufanya vitendo kama hivyo? Heshima yangu itakuwa wapi?” alihoji mama
Kanumba.
Mama
hakusita kutoa ufafanuzi zaidi juu ya madai hayo kwenda mbele hadi
kufikia hatua ya kudai kuwa anaonekana na dogodogo huyo katika maeneo
tofauti.
“Wanasema
nimekuwa nikionekana naye sehemu tofauti? Inawezekana akawa ni huyu
mwanangu Hotma Peter ambaye nimekuwa nikishirikiana naye kwenye kazi
mbalimbali kwa kuwa watu hawamjui na walizoea kuniona nikiwa na Seth
Bosco (mdogo wa marehemu), ukweli sina bwana na wala sihitaji hata awe
pedeshee wa aina gani,” alisema mama Kanumba.
Moja ya filamu aliyocheza Mama Kanumba(Flora Mtegoa)
Akizungumzia
kuhusu kampuni ya Kanumba The Great Film aliyoiacha marehemu mwanaye,
mzazi huyo alisema kampuni hiyo kwa sasa bado inaendeleza shughuli za
filamu japo kipindi cha nyuma ilikuwa haipo bize sana kwa kuwa akili
yake haikuwa sawa.
“Kampuni
bado inafanya kazi, japo kwa sasa msemaji wa kampuni hiyo ni Hotma
ambaye ni mtoto wa marehemu mdogo wangu, Seth kwa sasa yupo bize na
mambo yake mengine japo tunashirikiana naye katika kuandaa kazi
mbalimbali na tumefanikiwa kutoa filamu moja mpaka sasa.
“Ukweli
ni kwamba Kanumba hakuacha kazi yoyote, kwa kuwa kazi zake zote
hatimiliki walikuwa nazo Kampuni ya Steps Entertainment na ya Mtitu, ni
vizuri wasanii wawe makini na hili angalau ziwepo na kampuni ambazo
hazina utaratibu wa aina hiyo wa kumiliki haki zote za kazi ya msanii,”
alifunguka bi mkubwa huyo.CHANZO GPL
0 comments:
Post a Comment