Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel.
*******
STAA wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel, amesema hakuna ukweli wowote wa
yeye kutanua na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu nchini
Marekani, kwani alikutana naye ukumbini, akiwa amealikwa na blog iitwayo
Vijimambo ambayo hutangaza utalii wa Tanzania nchini humo kila
mwaka.Alisema wakati wa safari yake hakuelewa lolote kuhusu
Waziri Nyalandu na anashangazwa na yanayozungumzwa hivi sasa kwani baada
ya kumsalimia walipokutana, hawakuwahi kuonana tena hadi aliporejea,
kwani yeye alikuwa amepangiwa kwenye hoteli ambayo pia ndiyo ukumbi wa
shughuli hiyo ulipokuwa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza jambo.
“Watu wanataka kunijengea uadui na mke wake Faraja Kota ambaye
tunaheshimiana sana, mimi nilialikwa kule nikiwa na wasanii wengine,
wanamuziki Kassim Mganga na IT na hata malipo ya kazi yangu nililipwa na
wao, wanaosema nilitumia hela za wizara sijui wanataka nini, kama
wizara iliwapa fedha hao waliotualika mimi sijui,” alisema muigizaji
huyo.
0 comments:
Post a Comment