Monday, September 29, 2014

ISABELA ASAKA GAUNI LA HARUSI

Isabela Mpanda.
KATIKA hali ya kushangaza na kuonyesha kwamba ana hamu ya ndoa, msanii wa filamu na muziki, Isabela Mpanda hivi karibuni alinaswa akitafuta gauni la harusi wakati hata vikao havijaanza.
Msanii wa filamu na muziki, Isabela Mpanda.
Kikizungumza chanzo makini kilisema mwanadada huyo alikuwa maeneo ya Makumbusho jijini Dar akipita kwenye maduka mbalimbali akitafuta gauni la harusi wakati hata maandalizi ya harusi yake na Luteni Karama hayajaanza.
Baada ya kuzinyaka habari hizo paparazi wetu alimtafuta Isabela ambapo alikiri kusaka gauni hilo na kudai anajiandaa kwa ndoa mwishoni mwa mwaka huu.
Luteni Karama akipozi.
“Nina hamu sana ya kuingia kwenye ndoa ndiyo maana naanza mapema, Mungu akijalia vikao vitaanza mwezi wa kumi, mwaka huu,” alisema Isabela.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI