Friday, September 19, 2014

DKT. SHEIN AMALIZA ZIARA YAKE NCHINI COMORO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Rais wa Serikali ya JamhurI ya Muungano wa Comoro Dr.Ikililou Dhoinine wakiagana katika ukumbi wa Ikulu ya Comoro wakati Rais Shein alipomaliza ziara yake na ujumbe aliofuatana nao nchini humo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Comoro Mohamed Ali Soilihi katika uwanja wa Ndege wa Comoro wakati Dk.Shein alipomaliza ziara yake ya siku nne nchini Comoro.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakiagana na Viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Comoro katika Uwanja wa Ndege wa Comoro baada ya kumaliza Ziara ya siku nne kwa mualiko wa Serikali hiyo.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu Zanzibar.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI