Mwigizaji ‘sexy’ mwenye mvuto kwenye tasnia ya filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Limekuwa ni jambo la kawaida kwa baadhi ya mastaa wa Kibongo kuonesha au kupiga picha anaponunua gari jipya huku suala la kuonesha kadi ya gari likiwa gumu na ahadi zisizokwisha lakini mwigizaji ‘sexy’ mwenye mvuto kwenye tasnia ya filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameandika historia ya tofauti.
KADI YA GARI
paparazi limenasa kadi ya gari jipya la Lulu aina ya Toyota Rav4 New Model lenye rangi ya silva hivyo kuthibitisha kuwa yeye si kama wale wanaohongwa magari bila kupewa kadi.
Habari zilidai kwamba Lulu ameamua kufanya hivyo ili kuwaziba midomo baadhi ya mastaa waliozoea kutembelea magari ya kuhongwa na wanaume.
DONGO KWA WEMA?
Ilisemekana kwamba ni dongo kwa mastaa wakubwa kama Wema Isaac Sepetu ambaye aliwahi kuhongwa gari la kifahari aina ya Audi Q7 na yule kigogo wake maarufu kwa jina la CK, kabla ya kunyang’anywa na kurudishwa kwa mwenyewe kwani lilikopwa.
AU JACK WOLPER?
Kuna madai kwamba pia kijembe hicho kilitupwa kwa Jacqueline Wolper Massawe ambaye naye aliwahi kuhongwa gari la kifahari aina ya BMW X6 na yule aliyekuwa bwana’ke, Abdallah Mtoro ‘Dallas’ ambalo hadi leo linaozea Majembe Auction kwa kuwa liliingizwa Bongo kimagumashi.
JE, NI AUNT AU KAJALA?
Kwa mujibu wa watu wake wa karibu, pia dongo hilo huenda lilielekezwa kwa mastaa wengine kama Aunt Ezekiel Grayson na Kajala Masanja ‘K’ waliowahi kuripotiwa kwa skandali ya kuhongwa magari huku wengine wakitamba na magari ya kukodisha wakidai ni yao.
LULU ATIRIRIKA
Baada ya kuinyaka ishu hiyo kutoka kwa chanzo makini, paparazi lilizungumza na staa huyo ambapo alisema kwamba amechoka kila kukicha kutangaziwa sijui pedeshee gani kamhonga gari, mara anakodisha magari atanulie mjini, jambo ambalo halina ukweli wowote.
LULU ANA HOJA
Lulu alitoa hoja kwamba ili kuvunja kasumba hiyo, ameamua kuweka kadi ya gari hilo hadharani ili na hao wenye kujitamba katika mitandao ya kijamii na magari yao ya kifahari, waweke hadharani kadi zao zinazoonesha umiliki wao wa halali.
“Mimi siyo Mswahili kama wengine ndiyo maana nimeonesha kadi yangu kutokana na maneno ya ajabu ya kila siku wanayonitangazia.
“Sasa nasema hivi, mimi nimeonesha kadi yangu na wao waweke hadharani kadi zao za hayo magari yao ya kifahari wanayoringia mjini tuone umiliki wao wa halali,” alisema Lulu ambaye ni staa wa kwanza Bongo kuonesha kadi yake ya gari inayomuonesha kuwa ni mmiliki halali.
Mbali na gari hilo ambalo mwenyewe anadai amelinunua dola 27,000 (takriban shilingi milioni 44), pia Lulu anamiliki nyumba anayoendelea kuijenga iliyopo maeneo ya Mbezi Shamba jijini Dar hivyo kuwafunika mastaa wengi wakubwa wa tasnia ya filamu Bongo.
0 comments:
Post a Comment