Sunday, August 10, 2014

*KALI YA MWAKA* NYANI AJIPIGA (SELFIE) PICHA KIBAO, MMILIKI WA KAMERA APATA WAKATI MGUMU

MTANDAO wa Wikipidia umekataa kufuta picha ambayo Nyani ilijipiga ikisema kuwa kwa sababu picha hiyo ilipigwa na Nyani ambaye ni mnyama wala sio binadamu, basi inakuwa mali ya umma.
Hii ni baada ya mpiga picha, mmiliki wa kamera iliyotumika na Nyani huyo kujipiga picha, kusihi Wikipedia kufuta picha hiyo na kudai kuwa Wikipedia ilikuwa inaingilia haki zake za umiliki wa picha hiyo.
Mpiga picha, David Slater, alikuwa akijaribu kunasa picha za Nyani kwa masaa kadhaa, wakati ambapo Nyani mmoja alichukua mojawapo ya kamera za David na kujipiga mamia ya picha.
Picha hiyo aliyojipiga Nyani bila shaka ni ya kusisimua na imempeleka David kuwa maarufu ulimwengu mzima.
La kusikitisha ni kuwa hatimaye Slater sasa amejipata katika mvutano wa kisheria na Wikimedia kuhusiana na ni nani hasa mmiliki wa picha hiyo.
David, ambaye hutegemea upiga picha kama jinsi moja ya kujikimu kimaisha, yuko makini kuhakikisha picha hiyo imeondolewa kwa tovuti ya Wikipedia mara moja, huku Wikipedia ikidai kuwa iwapo kuna mmliki wa picha hiyo basi ni Nyani aliyejipiga picha hiyo.
Mvutano wa kisheria ilirejelewa kuangaziwa kufuatia uamuzi wa Wikipedia kuchapisha maombi yote iliyopata kuhusu kufuta au kuhariri habari au picha au video zozote ilizoweka kwenye tovuti zao.

Mojawapo ya maombi hayo ni David Slater kutaka picha aliyojipiga Nyani kuondolewa kwenye tovuti ya Wikipedia mara moja kwani ikiwa kwenye tovuti hiyo iko wazi kwa umma.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI