Saturday, August 23, 2014

JERRY SLAA: UBOMOAJI KARIAKOO UNALENGA KUPISHA UJENZI WA BARABARA YA MABASI YAENDAYO KASI

Na Suleiman Msuya
WAKATI kukiwa na hali ya sintofahamu juu ya ubomoji wa mzumnguko wa uliopo katika makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi Kariakoo Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Meya wa Manispaa hiyo Jerry Slaa amesema ubomoaji huo unalenga kupisha ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi.
Meya huyo alibainisha hilo wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii jijini Dar es Salaam.
Alisema Mradi wa mabasi yaendao kasi unahusu barabara ya Morogoro, Kawawa na Msimbazi hivyo Manispaa inapaswa kuondoa ili kupisha ujenzi huo.
“Unajua Serikali ipo katika mkakati wa kuboresha miundombinu hivyo eneo lile la mzunguko wa Msimbazi linahusika hivyo tunapswa kuuondoa ili ujenzi uendelee”, alisema.
Slaa alisema pamoja na kuondoa mzunguko huo Manispaa inaendelea kutafuta eneo ambalo watauhamishia ili kuendelea kuonekana katika  Manispaa hiyo na jiji kwa ujumla.
Meya huyo Manispaa ya Ilala aliwataka wananchi wa Ilala na maeneo mengine ya Dar es Salaam wasiwe na hofu juu ya kinachoondelea kwani ni katika harakati za kuboresha jiji.
Akizungumzia juu ya changamoto ambazo zinaikabili Manispaa ya Ilala alisema ni suala la kuondoa uchafu katika makazi ya watu ambapo kata 16 kati ya 26 za manispaa hiyo bado hazijapata mzabuni wa kukusanya taka.
Slaa alisema Manispaa ipo katika mkakati wa kuzisaidia Kata zilizobakia magari ya kubeba taka ambapo kwa kuanzia watatoa magari tisa kwa vikundi ambavyo vipo katika kata.
“Changamoto zipo nyingi ila hii ya taka inatuumiza vichwa sasa hivyo tumefikiria ili kuondoa taratibu za wananchi kuweka taka barabarani tumeamua kuvipatia vikundi katika Kata magari ili wafanye kazi hiyo ya kukusanya moja kwa moja wenyewe”, alisema.
Pia alisema manispaa hiyo inakabiliwa na changamoto ya bajeti inayotosha, watumishi wachache ambapo pia walio wengi wanaelimu ndogo ambayo haindani na kasi ya mahitaji ya jamii.
Alisema juhudi za manispaa hiyo ni kuhakikisha kuwa jamii inapata huduma zilizo na vigezo na kwa wakati ili wawe ni sehmu ya maendeo ya manspaa yao.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI