Monday, September 7, 2015

JUX AELEZA SABABU ZA YEYE NA VANESSA KUKATAA KUFANYA SHOW NA INTERVIEW WANAZOITWA PAMOJA


JUX na Vanessa Mdee ni wapenzi, lakini mara nyingi huwa wanakataa kufanya show pamoja au kufanyiwa mahojiano ya Radio na TV pamoja kama ilivyo kwa couple zingine kama ya Nahreel na Aika wa Navy Kenzo, au ya Shilole na Nuh Mziwanda.
Wiki hii Jux alipokuwa katika kipindi cha Ala Za Roho cha Clouds Fm siku ya birthday yake akiwa na girlfriend wake Vanessa, alisikika akisema kuwa ni nadra sana wao kufanyiwa mahojiano ya pamoja au kufanya show pamoja.
Nimemtafuta Jux ili kutueleza sababu za kukataa kufanya show za pamoja au mahojiano ya pamoja kama couple.

Sababu ya kwanza ambayo Jux ameitoa ni kuwa wanataka watu waelewe kuwa wao ni wapenzi lakini sio kundi la muziki, ni brand mbili tofauti ambazo linapokuja swala la kazi huwa hawapendi kuwachanganya watu.

“hatutaki kutengeneza mazoea ya kufanya show pamoja kila sehemu kwasababu watu ndio wanavyotaka, hiyo itatengeneza iwe kama kundi itakuwa kama Navy Kenzo, Vanessa ni peke yake na mimi ni peke yangu.”
Ameongeza kuwa ikitokea muandaaji akiwataka wote kwenye show moja huwa wanatoza pesa nyingi zaidi ya zile ambazo hata wangetoza kama msanii mmoja mmoja.
“Lakini sio kwamba hatufanyi kabisa tunafanya lakini inakuwa kwa pesa nyingi zaidi , kwahiyo tunapokuwa tunafanya show za pamoja tunakuwa tuna charge zaidi. Kwasababu watu wengi sana wanachukua advantage wanasahau kama sisi ni wasanii tofauti, wanajua kama ni kundi sijui, halafu wengi wakipiga simu wanauliza unaweza kuja na Vanessa na wakimpigia Vanessa naye akipigiwa unaweza kuja an Jux sasa wanakuwa wanasahau mimi ni msanii tofauti na Vanessa yaani brand zetu ziko tofauti kuwa wapenzi na kazi ni tofauti kabisa.” – Jux

Hata hivyo Jux ameongeza kuwa licha ya kukwepa show za pamoja ili wasionekane kama kundi, lakini kuna nyimbo walizofanya pamoja na wanasubiri muda muafaka ukiwadia wataanza kuziachia. 


0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI