Monday, August 11, 2014

ANGALIA PICHA KIJANA HUYU ANAVYOTESEKA

JOSE Serrano ni mtoto wa Ciudad Juarez kutoka nchini Mexico. Jose mwenye umri wa miaka 11 sasa ana uvimbe ukubwa wa kutisha katika shingo yake na amelazimika kuishi na uvimbe huo kwa maisha yake yote. Alipo zaliwa uvimbe huo ulikua na ukubwa kiasi cha mpira mdogo, lakini umekua ukiendelea kukua siku hadi siku na sasa kufikia kama inavyoonekana kwenye picha.
Pamoja na kwamba uvimbe huo umekua ukitishia maisha ya mtoto huyo tangu ulupoonekana kwa mara ya kwanza, Madaktari wanasema hawakujua kama Jose angeweza kuishi hata siku 1 baada ya kuonekana nao alipokua mchanga. Kwa mujibu wa madaktari, uvimbe huo umezidi kua hatari zaidi sasa kwa maisha ya mtoto Jose na unaweza ukaanza kuathiri mfumo mzima wa upumuaji wa kijana huyu kwani umeanza kuingiliana na mfumo wa mapafu yake.
Hatahivyo wazazi wa mtoto huyo wanamshukuru Mmishonari mmoja aliyekua akifanya kazi katika shirika la kusaidia watoto yatima huko mjini Ciudad Juarez, nchini Mexico. Mmishenari huyo alimkutanisha Jose na madaktari na wataalam kutoka Hospitali ya watoto ya Chuo kikuu cha New Mexico, ambao wanaamini wamepata ufumbuzi wa tatizo hilo. Na katika hali ya kushangaza wanasema ufumbuzi huo ni vidonge aina ya VIAGRA!
Ingawa sote tunajua Viagra ni nini na vinafanya kazi gani, kila mtu anajiuliza inakuaje apewe mtoto wa miaka 11? Lakini madaktari wanasisitiza kua kazi nyingine au uwezo mwingine wa vidonge hivyo ambao haujulikani na wengi ni kutibu au kunyong’onyeza uvimbe kama wa mtoto Jose.
Pia Mmishenari ameweza kuanzisha mfuko wa kujitolea kuchangia ili kumwezesha mtoto huyo kulipia matibabu hayo, ambayo yanagharimu kiasi cha Dola 2,000 kwa wiki (sawa na Tsh. Mil 3.2) kwa ajili ya Madawa na Dola 125,000 (sawa na Tsh. Mil 200) kwajili ya Upasuaji na Matibabu. Pesa hiyo yote imefanikiwa kukusanywa kupitia michango kutoka Hospitalini, Kanisani na watu mbalimbali. Pia kampuni ya Pfizer ambayo inatengeneza vidonge wamejitolea kulipia gharama zote za vidonge Hivyo.
Jose mwenyewe anashangazwa na kufurahishwa na hayo na anatumaini kua matibabu hayo yatamwezesha kuishi maisha ya kawaida. “Kama madaktari watafanikiwa kunitibu, nitafurahi sana. Nitakua na furaha na nitaweza kuishi maisha ya furaha na kufanya kilakitu ninachotaka.” Alisema mtoto Jose kwa hisia kali.
Share habari hii, kisha andika “AMEN” kwenye comment kama unamtakia mafanikio mtoto Jose katika matibabu yake.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI