Thursday, July 17, 2014

UWOYA BHANA! AFANYA FUJO KUBWA NYUMBANI KWA MUME WA MTU!!! TIRIRIKA NA KISA KIZIMA HAPA!

Stori: Shakoor Jongo
NYOTA wa sinema za Kibongo, Irene Pancras Uwoya amesababisha tena! Safari hii amekinukisha nyumbani kwa mwanaume aliyewahi kuwa mpenzi wake (jina tunalo)
kufuatia jamaa huyo kufunga ndoa na mwanamke mwingine na kumfanya Uwoya kuendelea kuwa ‘nyumba ndogo’. Kwa mujibu wa chanzo chetu, ishu hiyo ilichukua nafasi juzikati, nyumbani kwa mwanaume huyo, Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.

MCHEZO ULIVYOKUWA
Chanzo kilidai kwamba, siku ya tukio, Uwoya akiwa na baadhi ya mastaa wenzake (hawakutajwa) kwenye kambi ya maandalizi ya kurekodi filamu mjini Bagamoyo, Pwani, alipokea simu iliyomnyetishia kuwa, mpenzi wake huyo amefunga ndoa na mwanamke mwingine jijini Mwanza, kwa hiyo yeye aliye tu!

UWOYA ACHANGANYIKIWA
“Uwoya alipopata salamu hizo kwa njia ya simu alichanganyikiwa! Alianza kusema maneno ya kumshutumu waziwazi huku akiangua kilio. Mbaya zaidi aliyemjulisha ishu hiyo alisema ndoa hiyo ilishafungwa na si kwamba ipo kwenye maandalizi.
“Akasema anaondoka kambini kumfuata jamaa yake na kwamba atamtambua kwani nia yake ilikuwa kwenda nyumbani kwake kumfanyia fujo na huyo mke mpya,” kilisema chanzo hicho cha uhakika.

AANZIA DUKANI
Chanzo kilizidi kudai kwamba, licha ya wasanii wenzake kumsihi asichukue hatua hiyo anaweza kuishia polisi, Uwoya hakukubali, aliondoka kwa hasira na breki yake ya kwanza ilikuwa kwenye duka kubwa la jamaa huyo lililopo Mikocheni, Dar ambapo alifanya fujo.
“Kule alipogundua huyo mwanaume wake hayupo ndiyo akaondoka hadi nyumbani kwake, Sinza ambako aliendeleza fujo zake kwa kutukana na kutishia mambo mengi,” chanzo kilisema.

HASIRA PEMBENI
Kwa mujibu wa chanzo, ni dhahiri kuwa, Uwoya aliondoka eneo hilo baada ya kuanza ‘kujaza nzi’ (watu kuwa wengi) ambapo aliondoka mdogomdogo na kama hana hasira utadhani si yeye aliyekuwa akichafua hali ya hewa.

MATEGEMEO YAKE
Habari za ndani ziliendelea kudai kuwa, Irene alishikwa na hasira za jamaa huyo kuoa kwa vile alikuwa akiamini zali hilo lingetua kwake baada ya ndoa yake na msakata kabumbu wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Katauti’ kwenda halijojo!
“Uwoya alitegemea angeolewa yeye, sasa kusikia jamaa kaoa mwanamke mwingine tena kwa siri, ilimfanya aishiwe nguvu,” kilisema chanzo.

ALICHOAMINI
Habari zinazidi kudai kwamba, alichoamini Uwoya ni kwamba kitendo cha mwanaume huyo kuoa kingemfanya yeye aendelee kuwa ‘nyumba ndogo’ jambo ambalo hakupenda kulisikia hata kidogo.

UWOYA HUYU HAPA
Baada ya gazeti hili kunyetishiwa filamu nzima, lilimsaka staa huyo na kubahatika kukutana naye maeneo ya Sinza Palestina jijini Dar ambapo alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba, alishaachana na mwanaume huyo.
“Ilitokea, lakini nilishaachana naye. Unajua ishu si kwamba angenioa mimi, ila kitendo alichokifanya hakikuwa cha uungwana,” alisema Uwoya.

AMWANGA CHOZI
Katika hali isiyotarajiwa, msanii huyo alianza kumwaga chozi bila kusema sababu hata pale alipoulizwa kama chozi hilo lilitokana na kukumbuka tukio la jamaa yake kufunga ndoa kwa siri au la!
Uwoya: “We niache tu, nina mambo mengi sana yanayoniliza mimi.”
Kwa upande wake mwanaume huyo alipopatikana kwa njia ya simu na kueleza ishu nzima alijibu kwa kifupi: “Haiwahusu.” Kisha akakata simu.

HISTORIA
Uwoya na Ndikumana walifunga ndoa Julai 11, 2009 kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Mei 8, 2011 walijaliwa kupata mtoto wa kiume aitwaye Krish.
Hata hivyo, Novemba 16, 2011 kwenye gazeti hili kuliandikwa habari yenye kichwa;

NDOA YA UWOYA YAVUNJIKA
Ndoa hiyo iliparaganyika baada ya Uwoya kudaiwa kumkataa mwanaume huyo na mpaka sasa haijasimama tena huku mwanaume akiwa kwao, Rwanda.
Na GP

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI