MWANAMKE mmoja wa Kitanzania aliyefanya ukabaha kwa miaka 18 katika miji mbalimbali ya Tanzania, likiwemo Jiji Kuu la kibiashara la Dar es Salaam na mingine ya Namibia, ameibuka na kueleza jinsi alivyotenda dhambi ya kusambaza Ukimwi kwa wanaume wakware.
Licha ya kukiri kufanya hivyo, akisema kwa siku alipanga hadi wanaume watano, tena bila ya kutumia kinga akisema alidhamiria kuusambaza ugonjwa huo hatari alioambukizwa akiwa katika shughuli za ukahaba.
Alijigundua ameathirika mwaka 2006.
Hata hivyo, katika maelezo yake ameelezea kuijutia dhamira yake hiyo, akisema alisambaza kutokana na hasira aliyokuwa nayo dhidi ya mwanamume aliyemwambukiza.
“Nilimchukia sana kila mwanamume, yeyote aliyejiita mwanamume… nilishindwa tu kuwawinda na kuwaua, lakini dhamira yangu ilikuwa kutumia silaha yoyote kuua wanaume kwa sababu mmoja wao aliniua…
“Ndani mwangu nilijisemea kamwe sitawaambia hali ya afya yangu, yeyote anayekuja kwangu nammaliza. Kwa namna walivyoniambukiza lazima niwaambukize’.
"Sijui nimewaambukiza wanaume wangapi, lakini ni maelfu,” alisema mwanamke huyo ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 32, alipotoa ushuhuda wake kanisani nchini Nigeria hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment