Tuesday, July 22, 2014

MUAROBAINI KWA WANAOVAA NUSU UCHI VYUONI HUU HAPA! SOMA ZAIDI…!

SERA ya kudhibiti mavazi yasiyoendana na maadili, yanayovaliwa na wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini, inaelezwa itakuwa muarobaini kwa wanafunzi husika.
Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara (MUCCoBS) cha Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Profesa Faustine Bee, alisema serikali ipo katika mchakato wa kuanzisha sera hiyo ambayo wanaamini itakuwa msaada mkubwa wa kulinda uvaaji vyuoni.
Alisema kuwa chuo hicho pamoja na vyuo vingine haviwezi kuwaruhusu wanafunzi, hasa wa kike kuvaa mavazi ya nusu uchi yanayoshushia heshima vyuo na utu wa wahusika.
Prof. Bee alisema kuwa pamoja na sera hiyo kuwa hatika hatua za mwisho, walengwa ambao ni wanafunzi, nao watashirikishwa ili kutoa maoni yao juu ya mfumo stahiki wa mavazi hayo na kuongeza wakubali wasikubali sera hiyo ni mhimu kwa lengo la kudumisha heshima ndani ya jamii.
Alisema suala la nidhamu ni muhimu kwa lengo la kujenga maadili mema ndani ya jamii na kuongeza kuwa vijana wengi  wamejiunga na vyuo wakitokea kwa wazazi wao, lakini wamekuwa na uhuru wanaoutumia vibaya.
Prof. Bee alisema kama vijana wataendelea kulelewa kwenye maadili mema, taifa litakuwa na kizazi chenye staha.
Kwa mujibu wa Prof. Bee, mchakato wa sera hiyo ya mavazi ukikamilika utarasimishwa rasmi na mwanafunzi atakayeikiuka ataondolewa chuoni hapo.
Katika hatua nyingine, chuo hicho kimekaribisha wawekezaji watakaojenga hosteli na sehemu za chakula kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya wanachuo na wafanyakazi wake.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI