Friday, July 18, 2014

MADINI YENYE THAMANI YA BILIONI 10 YAPORWA KATIKA KAMPUNI YA TANZANITE ONE

WATU wanaosadikiwa ni majambazi wamepora madini ya tanzanite ya Kampuni ya TanzaniteOne ya Mirerani, wilayani Simanjiro, mkoani Manyara yenye uzito wa kilo 40 na thamani ya zaidi ya Sh bilioni 10.
Taarifa kutoka katika kampuni hiyo zilisema, uporaji huo ulitokea jana ndani ya kampuni hiyo saa tisa usiku.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Dauglas Swartz, tayari wafanyakazi watano wa kampuni hiyo wanashikiliwa na polisi katika kituo kidogo cha Mirerani kuhusu wizi huo.
Alisema jana kwa njia ya simu kuwa, Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Manyara (RCO), Benedict Msuya alifika eneo la tukio kwa uchunguzi wa wizi huo.

“Ni kweli tumeibiwa madini ya tanzanite na baadhi ya wafanyakazi wanaodaiwa kuhusika katika tukio hilo wameshakamatwa na upelelezi bado unaendelea, niache kwa sasa,’’ alisema mkurugenzi huyo.
Taarifa zilizopatikana ndani ya kampuni hiyo zinadai kwamba madini hayo yaliyokuwa yamefungwa katika mifuko miwili tofauti yenye uzito wa kilo 15 na kilo 25 na yameporwa mita chache kutoka mgodini eneo la kuingia chumba cha ulinzi.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI