Wednesday, July 23, 2014

JAMES RODRIGUEZ AKABIDHIWA JEZI NAMBA 10 REAL MADIRD NA KUPIGA SHOO LA HATARI BERNABEU

Amesajiliwa: James Rodriguez ametambulishwa Real Madrid leo na kukabidhiwa jezi mamba 10 Uwanja wa Santiago Bernabeu

MFUNGAJI bora wa Kombe la Dunia, James Rodriguez hatimaye ametambulishwa Real Madrid baada ya kukamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 60 kutoka Monaco jioni ya leo.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Colombia amesaini mkataba wa miaka sita na Madrid baada ya kufuzu vipimo vya afya asubuhi Santiago Bernabau na kukabidhiwa jezi namba 10.
Rais wa Madrid, Florentino Perez amemkaribisha mshambuliaji huyo akimfananisha na gwiji wa zamani wa klabu hiyo, marehemu Alfredo Di Stefano ambaye pia alijiunga na klabu hiyo akitokea Colombia. 
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez (kushoto), Rodriguez (kulia) na mkewe Daniela wakati wa kutambulishwa
Rodriguez akionyesha uwezo mbele ua maelfu ya mashabiki uwanjani
Rodriguez alionyesha uwezo mkubwa Bernabeu
Rodriguez alikonga nyoyo za mashabiki kwa vita hivi

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI