NAFASI ya muziki wa Tanzania kupenya inazidi kuonekana na hii ni baada ya wasanii kadhaa akiwemo Diamond na Shettah kufanya video na Director God Father huyu anaingia kwa list ya wasanii waliopata nafasi ya kumulikwa na kamera za muongozaji God Father.
Wiki chache Linah alianza kupost vipande vya picha na video ambayo wengi tulikua tukiona tu maandishi yanayosema inakuja,leo baada ya futari THT Linah ameitumia nafasi hiyo kutambulisha rasmi video na audio ya wimbo huu.
Mtu wa kwanza kuinunua video hii ambaye ameingia kwa rekodi ni Cloud kutoka Bongo Movie ambaye alipoiona tu akatoa pesa akainunua,wapili ni Mrisho Mpoto ambaye nae hakutaka kusubiri zaidi.
Linah ameagwa rasmi na uongozi wa THT baada ya kupata uongozi mpya utakaoanza kumsimamia kazi zake ambazo kwa utangulizi wameanza na kazi hiyo iliyofanyika South Africa kuanzia audio hadi video na kampuni hiyo inaitwa No Fake Zone Entartainment.
Bonyeza play kusikiliza nyimbo na kui-download.
Bonyeza play kuitazama video hii. Enjoy!!!
0 comments:
Post a Comment