Sunday, June 22, 2014

RIPOTI KAMILI: AJALI YAUA WATU SITA PAPO HAPO NA KUJERUHI WENGINE 16 BARABARA YA BAGAMOYO



    1. Picha na Habari
    2. Na Frank Mavura, Dar es salaam
    3. ******************
    WAKAZI wengi waishio kando kando ya barabara ya Bagamoyo Jijini Dar es salaam ameendelea kuilalamikia serikali kuweka matuta katika barabara hiyo ambayo imeonekana kuwa ni chanzo cha ajali nyingi  zinazopelekea vifo na wengine kupata ulemavu wa kudumu.
    Hilo limeendelea kujidhihirisha katika ajali iliyotokea katika barabara ya Bagamoyo iliyoua watu sita na kujeruhi wengine 16.

    Ajali hii imetokea majira ya mchana ambapo imehusisha jumla ya magari manne ikiwemo daladala mbili, gari ndogo moja na lori, iliyotokea eneo la Makongo karibu na hospitali ya Lugalo Dar es salaam ambapo mashuhuda wamesema ajali hiyo imekuwa ni miongoni mwa ajali mbaya kutokea katika mwaka huu, huku wakilaumu kuwa imesababishwa na uzembe uliofanywa na dereva wa daladala iliyokuwa ikitoka Tegeta kwa kupita upande ambao sio wake.

      IMG-20140621-WA0006
      Daladala iliyopata ajali na kusababisha vifo vya watu sita na wengine kujeruhiwa
    1. IMG-20140621-WA0003
      1. Lori lililomkanyaga mmoja wa abiria baada ya kurushwa nje toka katika Daladala hiyo.
      2. Gari ndogo aina ya Landrover iliyogongwa ubavuni na daladala.
      3. Katika kuhakikisha kuwa tunakuhabarisha ULIMWENGU WA HABARI ilitembelea katika hospitali ya  jeshi ya Lugalo ambapo majeruhi na miili ya watu waliofariki ilifikishwa  Hospitalini hapo, na kujionea hali halisi ilivyokuwa.
      4. Brigedia general Makere Josiah ambaye ni mganga mkuu wa hositali ya lugalo amethibitisha idadi ya majeruhi na idadi ya watu waliopoteza maisha.
      5. Madaktari wakijaribu kuyaokoa maisha ya kijana mmoja ambaye alikuwa ni majeruhi wa ajali hiyo.
3
Gari ndogo ikiwa imebeba miili ya watu waliofikwa na umauti katika ajali hiyo
  1.  
  2. Simanzi ilitawala nje ya hospitali ya Lugalo ambapo familia hii ilimpoteza kijana wao wa kiume.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI