Tuesday, June 17, 2014

NJIA MPYA INAYOTUMIKA KUTAHIRI WANAUME UGANDA! CHEKI PICHA HIZI!!!

mpira2
Wizara ya afya nchini Uganda imeanza majaribio ya kutumia kifaa kipya kwa ajili ya kutahiri wanaume ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Kifaa hicho rahisi cha mpira kinatumika kutoa ngozi ya mbele ya uume wa mwanaume tofauti na mwanzo ambapo kisu kilikuwa kikitumika kufanya shughuli hiyo.
mpira
Igalla ambaye ni baba wa watoto wawili amefanyiwa tohara kwa kutumia njia hiyo ambapo anasema inachukua dakika chache na hakujihisi vibaya hata kidogo tofauti na tohara za kimila ambapo mwanaume hutahiriwa kwa kutumia kisu.
Wanasayansi waligundua kuwa tohara kwa wanaume inaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Mbali na Uganda kifaa hicho pia kinatumika nchini Botswana, Kenya, Mozambique, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe na nchi nyingine.
Uganda ina matumaini kuwa kifaa hicho kiitwacho PrePex kitawahamasisha wanaume wakubwa Uganda kwenda kufanyiwa tohara kama sehemu ya mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa Ukimwi unaosababisha vifo vya mamilioni ya watu.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI