Tuesday, June 17, 2014

NAFASI ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO 2014 ZATANGAZWA RASMI - 16800 WAKOSA NAFASI

 NAFASI za kujiunga na kidato cha nne mwaka 2014  kwa wanafunzi waliomaliza mwaka jana zimetangazwa rasmi muda huu jijini dar es Salaam na naibu waziri wa TAMISEMI  Bw KHASIM MAJALIWA  ambapo zaidi ya wanafunzi 16800 wamekosa nafasi hizo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo upungufu wa shule za kidato cha tano.
       Akitangaza majina na shule walizopangiwa wanafunzi hao Mh MAJALIWA amesema kuwa jumla ya wanafunzi 54085 sawa na alimilia 75.61 ya wanafunzi 71527 waliostahili kuingia kidato cha tano mwaka huu wamechaguliwa huku wavulanai ni 31352 wakati wasichana ni 22733 ambapo ni sawa na ongezeko la wanafunzi 20402 kwa kulinganisha na wanafunzi 33683 waliochaguliwa mwaka jana.
  Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na shule mbalimbali wataanza kuripot katika meneo yao tarehe 10 julai mwaka huu ambapo mwisho wa kufika katika shule walizopangiwa ni tarehe 30 julai mwaka huu ambapoamesema kuwa kwa wale ambao watakuwa hawajiripot hadi tarehe hiyo nafasi zao zitajazwa na waliokosa nafasi.
 Chanzo: matukiotz.com

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI