Askari wa jeshi la Polisi akichukua mwili wa marehemu baada ya ajali.
Baadhi ya majirani wakishuhudia uokoaji wa ajali ya moto.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilomba, Amir Kitululu akizungumza jambo akiwa katika eneo la tukio.
Baadhi ya vitu vikiwa vimenusurika kutokana na ajali hiyo.
Mama mzazi wa Marehemu, Winfrida Sokon akiwa anashangaa bila kuamini kilichotokea baada ya moto kumwangamiza mwanaye.
MTOTO mwenye umri wa miaka
Mitatu na nusu aliyefahamika kwa jina la Rehema Patrick amefariki dunia baada
ya chumba alichokuwa amelala kuteketea kwa moto.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mbeya, Ahmed Msangi, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa
limetokea leo asaubuhi majira ya saa moja asubuhi huko katika Mtaa na kata ya
Ilomba jijini Mbeya.
Amesema chanzo cha moto huo
hakijafahamika ambapo mtoto huyo ambaye ni marehemu alikuwa amelala wakati mama
yake mzazi aliyefahamika kwa jina la Winfrida Sokon (30), alikuwa ameenda
kuchota maji huku naye baba yake akiwa safarini.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa
Mtaa, Amiri Kilulu, amesema Mama huyo ni mgeni amehamia jana tu akiwa na watoto
wawili ambao ni Tukulamba Mwakyami(4) pamoja na marehemu, lakini huyo
mkubwa ndiye aliyegundua moto huo.
Amesema mtoto huyo baada ya
kugundua moto huo alimfuata mama yake alikokuwa akichota maji lakini walipofika
walikuta mtoto ameshafariki dunia ambapo majirani walijaribu kuuzima bila
mafanikio.
Jeshi la polisi lilifika eneo
la tukio na kuondoka na marehemu kwa ajili ya uchunguzi zaidi huku majirani nao
wakichangishana fedha kwa ajili ya kusaidia mazishi kutokana na ugeni wa
mwanamke huyo.
NA MBEYA YETU
0 comments:
Post a Comment