Sunday, June 22, 2014

MSIBA MKUBWA WAWAPATA YAYA NA KOLO TOURE WAKIWA NCHINI BRAZIL

article-0-1EC70F5000000578-221_634x444
MASAA kadhaa baada ya timu ya Ivory Coast kupokea kipigo cha magoli 2-1 kutoka kwa Colombia katika mchezo wa kundi C kwenye michuano ya kombe la dunia, mastaa wa timu Yaya na Kolo Toure wamepata habari mbaya zaidi.

Wachezaji hao wanaokipiga katika klabu ya Manchester City ya England, walipokea taarifa ya kifo cha  mdogo wao wa kiume ambaye pia ni mwanasoka.
Msiba huo mkubwa kwa Yaya Toure pamoja na kaka yake Kolo Toure umetokea jana jijini Manchester ambapo mdogo wao Oyala Ibrahim Toure alifariki akiwa hosptali The Christie akipewa matibabu baada ya kuugua saratani.
OYALA
Ibrahim Toure

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI