Hii ni nyingine toka nchini Kenya ambapo Julius Kepkoitch anaripoti kwamba baada ya kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab cha Somalia kutoa onyo kwamba mashambulizi yake yanayofata yatawahusu viongozi wa Kenya, imebidi system ya ulinzi wa rais kwenye msafara ibadilike.
Unaambiwa mabadiliko yalianza kuonekana toka mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye sherehe za 51 za kujitawala ambapo badala ya Rais kutumia gari aina ya Land rover iliyo wazi iliyokua pia ikitumika na marais wa awali, rais aliiingia kwenye uwanja wa michezo wa nyayo na gari aina ya Land cruiser iliyo na vioo visivyo penya risasi.
Hiyo Land Cruiser ililoongozwa na gari lenye mitambo iliyo na uwezo wa kugundua bomu kwa zaidi ya kilomita 10, nyuma kabisa kulikua na gari lililo na uwezo wa kuhimili risasi na bomu au kilipuzi cha aina yoyote na inasemekana kwamba gari hilo huwa linatumika endapo msafara wa Rais umeshambuliwa kwa haraka Rais na wakuu wengine wanaondolewa na gari hilo.
0 comments:
Post a Comment