Sunday, June 1, 2014

KAMPUNI YA APPLE YATHIBITISHA KUINUNUA BEATS BY DR DRE

Bidhaa za kamuni ya Apple pamoja na bidhaa za beata by dr dre.
Bidhaa za kamuni ya Apple pamoja na bidhaa za beata by dr Dre.
Hatimaye kampuni ya kielektroniki ya Apple imethibitisha kuwa itanunua kampuni ya Beats Electronics watengenezaji wa headphones za Beats by Dre na bidhaa nyingine za muziki inayomilikiwa na mwanamuziki Dr. Dre.
Ununui huo utakuwa na thamani ya jumla ya dola bilioni 3 ambapo inadaiwa kuwa ndio dili kubwa zaidi kubwa ya manunuzi kuwahi kufanywa na kampuni ya Apple.
Ikiwa ni sehemu ya manunuzi, wagunduzi wa kampuni hiyo Jimmy Iovine na Dr Dre wataungana na kampuni ya Teknolojia duniani Apple. Bosi wa kampuni ya Apple Tim Cook amesema dili hiyo itaruhusu kampuni ya Apple kutengeneza bidhaa nzuri zaidi za muziki

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI