Tuesday, May 27, 2014

SOMA HISTORIA FUPI YA MSANII WA BONGO MOVIE RECHO ALIYEFARIKI DUNIA, BAADA YA KUJIFUNGUA!

Historia Yake Fupi Hii hapa;
Rachel alizaliwa Mkoani Ruvuma
kwenye wilaya ya Songea na kupata
elimu yake katika Shule ya
msing Luida iliyopo wilayani hukohoko
Songea.

Baada ya Muda alihamia Dar essalaam
na kusoma shule ya sekondari ya
Baptist iliyopo
magomeni na baadaye kwenda
kumalizia elimu yake ya sekondari
katika Hanga.

Baada ya hapo
Rachel alijiunga na chuo cha Magogoni
kilichopo Jijini Dar es salaam katika
kujiendeleza zaidi
kielimu.

Rachel mara nyingi amekuwa
akizungumziwa na vyombo mbalimbali
vya habari hasa kutokana na mavazi
yake.

Enzi za uhai wake alipendelea kuvaa nguo fupi
ambazo huonesha vizuri umbo lake na
mara nyingi amekuwa ni kivutio kwa
watu wengi anapoonekana kwenye
matukio mbalimbali kwani wengi
hutugemea kumwona akiwa ndani ya
NGUO FUPI.
Katika moja ya interviews zake Rachel
aliwahi kusema kuwa hupendelea
kuvaa nguo fupi
kwani humfanya ajisikie huru na amani
pindi anapofanya shughuli zake.

Akiwa mmoja wa waigizaji wa kike
ndani ya Bongo Movies na mwenye
umbo lenye mvuto.

Rachel Haule ama "Recho" kama
anavyofahamika na mashabiki wake ni
mwigizaji aliyekuja kwenye tasnia ya
filamu miaka ya
karibuni na kuweza kujipatia umaarufu
kupitia filamu mbalimbali alizoigiza....

Historia ya Rachel katika maigizo
inaanza rasmi Mwaka 2009 katika
kikundi cha maigizo cha mburahati.
Baada ya kukaa kwenye kikundi
hicho ndipo alipojiingiza rasmi kwenye
uigizaji wa Filamu.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI