Tuesday, May 20, 2014

SHIWATA WAMLILIA NGALUMA, KUAMBIANA

Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)
Press Release

MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)umepokea kwa majonzi kifo cha mwanamuziki mashuhuri na maarufu wa mwanamuziki wa dansi nchini,Amina Ngaluma “Japanese” aliyefariki nchini Thailand.
Marehemu Ngaluma aliyekuwa mwanachama wa SHIWATA atakumbukwa kwa mengi mazuri aliyoyafanya akiwa mwanamuziki wa kike mwenye kipaji cha kutunga,kuimba na kutawala jukwaa katika maonesho ya akiwa na bendi mbalimbali ikiwemo Tam Tam, Double M,Tanzania One Theatre (TOT).
Ngaluma pia amewahi kufanya maonesho katika bendi za nje ya nchi kama Kenya na Thailand ambako amepatwa na mauti akiwa akifanya maonesho katika moja ya hoteli za kitalii.

SHIWATA inachukua nafasi hii kutoa pole familia ya Mzee Ngaluma kwa kuondokewa na mtoto wao mpendwa ambaye mbali ya mchango wake ulisaidia familia yake lakini pia taifa limepata pengo kwani alitumia kipaji chake cha sanaa kuelimisha, kuburudisha na kuitangaza Tanzania ndani na nje ya nchi.
Mtandao pia unaungana na familia ya msanii wa Bongo Movie, Adam Kuambiana katika msiba uliomkuta juzi wakati mchango wake bado unahitajika katika fani hiyo.
Mchango wa Kuambiana umeacha pengo kubwa katika tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa uwezo mkubwa aliokuwa nao wa kuigiza na kuongoza filamu alizowahi kucheza kama ya Salt.
Peter Mwenda
Ofisa Habari wa SHIWATA

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI