Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Said Meck Sadiki, amewataka wananchi wa mkoa huo wanapohisi wana dalili za ugonjwa wa dengue kuwenda katika hospitali za Serikali kwa kuwa matibabu hutolewa bila malipo.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuulizwa swali juu ya gharama kubwa za matibabu ya ugonjwa huo, kwenye ukumbi wa mkutano wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dares Salaam.
“Tunaomba wananchi wanapohiisi dalili za ugonjwa huo kwenda katika hospitali za Serikali ,ambazo ni Amana, Mwananyamala na Temeke kwa kuwa matibabu yanatolewa bila malipo” alisema Sadiki.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamwaja alisema vituo vyote vya Serikali vinapaswa kutoa matibabu ya ugonjwa huo bila malipo kwa kuwa ugonjwa huo ni mlipuko na magonjwa ya milipuko matibabu yake hutolewa bila malipo.
Mwamwaja pia alisema ikitokea hata vituo vya afya vya binafsi vikapewa vitenganishi na vifaaa vya tiba na Serikali navyo vinasapwa kutoa matibabu ya ugonjwa huo bila malipo.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kwa sasa wanajenga uwezo ili kila wilaya iwe na vituo vitano kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa huo.
Sadick aliongeza kuwa Serikali itanyunyuzia dawa ya (Lavacide) sehemu za mikusanyiko kama vile mashulenina kwenye madimbwi, lakini maeneo ya hotelini na mabaa watapaswa kunyunyuzia dawa kwa gharama zao.
“Kwa upande wa wizara, idara na taasisi za Serikali wanapaswa kunyunyuzia dawa kwa gharama zao,(yaani matumizi mengineyo)” alisisitiza huku akisema hata kwenye ofisi yake wamefanya hivyo kwa gharama zao.
Aidha Sadiki aliwataka viongozi wa mitaa na watendaji wengine kuwahimiza wananchi kuhusu usafi wa mazingira ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo.
Alisema wananchi wanapaswa kuhakikisha vifuu vya nazi visoda kwani maji kidogo yanayokaa katika vitu husababisha mbu wanaosabbaisha ugonjwa huo kuzaliana, hivyo vinatakiwa visitupwe ovyo na kufunika maji safi wanayoyahifadhi.
Alisisitiza hatua ya kwanza kuzuia ugonjwa huo ni usafi wa mazingira,hivyo dawa ni hatua ya mwisho.
|
Sunday, May 18, 2014
SERIKALI IMESEMA MATIBABU YA HOMA YA DENGUE NI BURE
10:36 AM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ZILIZOSOMWA ZAIDI
-
RAIS Mteule wa Marekani Donald Trump amepanga kufuta bajeti ya ununuzi wa ndege mpya ya Air Force One ambayo hutumiwa na marais wa nchi ...
-
SALUM MWALIM, JOHN MNYIKA NA DK SLAA Uchaguzi ndani ya chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA umefika tamati kwa kamati kuu ya cha...
-
KUPIGA punyeto kwa muda mrefu ni moja kati ya vyanzo vikuu vya tatizo la la ukosefu wa nguvu za kiume. Asilimia kubwa ya vijana wenye ta...
0 comments:
Post a Comment