Friday, May 23, 2014

R.I.P MAXMILLIAN NGUBE, SHUJAA WA KAMERA MLIMANI TV, UTAKUMBUKWA DAIMA

Wingu zito latanda baada ya tasnia ya habari kupokea kwa uchungu na masikitiko makubwa, kifo cha mzee wetu Max aliyejulikana zaidi kama papaa Max.
Alikuwa ni mfanyakazi hodari kutoka Mlimani TV, hakika wanamlimani na wapenzi wa tasnia ya habari kwa ujumla wamemkosha shujaa, kipenzi cha wengi na msema kweli,
Alikuwa ni mpiga picha hodari wa Mlimani TV kwa muda mrefu sana, Tutakukumbuka daima.
Alipenda kujulikana kama papaa Max na msiba utakuwa nyumbani kwa marehemu maeneo ya tegeta, mtandao huu utaendelea kukujuza juu ya mengi kuhusiana na mpiga picha huyu maarufu.
endelea kuwa nasi…!
Mungu ailaze Roho ya marehemu Maximillian Ngube mahara pema peponi. Amina



ULIMWENGU WA HABARI unawapa pole wote walioguswa kwa namna moja ama nyigine na msiba huu, familia, wafanyakazi wote wa Mlimani, wanafunzi wa shule kuu ya uandishi wa habari na mawasiliano kwa umma

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI