Wednesday, May 21, 2014

FIGO: HISPANIA HAITABEBA KOMBE LA DUNIA MWAKA HUU, NADHANI BRAZIL WANASTAHILI

Nyota wa zamani wa kimataifa wa Ureno, Luis Figo amesema Hispania haitabeba kombe la dunia mwaka huu.
FIGO aliyeichezea Ureno mechi 125 na kufunga zaidi ya magoli 30 amesema kikosi cha Vicente del Bosque hakina ubora wa kutetea ubingwa wao.
Hispania imeshinda makombe makubwa matatu mfululizo kati ya mwaka 2008 na 2012, japokuwa walipigwa na Brazil kwenye mechi Confederation Cup mwaka jana.
“Sidhani kama Hispania watashinda kombe,” Figo aliuambai mtandao wa Laureus.com. “ Sidhani kama wana ubora wa kufanya hivyo. Itakuwa vigumu kwao kushinda, lakini sio kwamba haiwezekani”.
Badala yake Figo amewapa nafasi Brazil kutwaa ubingwa mwaka huu kwasababu wana kocha bora na faida ya kucheza nyumbani.
“Nadhani inasaidia kucheza nyumbani. Namjua vizuri kocha wa Brazil (Luis Felipe Scolari) na naamini ni kocha bora kwa mashindano kama haya na nchi itaisaidia timu yao”. Aliongeza Figo.
“Itakuwa ngumu sana kwa timu zitakazocheza na Brazil 
(kwasababu ya sapoti).”
Kiungo huyo mstaafu alisema timu yake ya Ureno itahangaika sana kufika hatua za juu za mashindano kwasababu inamtegemea zaidi Cristiano Ronaldo.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI