Tuesday, May 27, 2014

BRENDAN ROGERS ASAINI MKATABA MPYA LIVERPOOL, AJIFUNGA MPAKA 2018

Mkataba mpya: Brendan Rodgers amesaini mkataba mpya unaomuweka Liverpool mpaka 2018
BRENDAN Rodgers amepewa ofa nzuri ya kazi katika klabu ya Liverpool kwa kusaini mkataba mwingine utakaomfanya akae muda mrefu zaidi Anfield.
Rodgers, aliyebakiwa na miezi 12 katika klabu hiyo amepewa zawadi hiyo ya mkataba baada ya kufanya vizuri ligi kuu na sasa amemwaga wino katika mkataba mpya unaosemekana kumuweka Merseyside mpaka 2018.
Liverpool walimaliza pointi mbili tu nyuma ya mabingwa Man City tangu mwaka 1990 na walionesha kiwango kikubwa mno chini ya Rodgers na kuwavutia Wamiliki wa klabu hiyo, raia wa Marekani.
Tangu Rodgers ajiunge na Liverpool 2012 akitokea Swansea City amekuwa kivutio kwa mashabiki na wamiliki wa klabu hiyo na sasa wanajiandaa kumpa dau la kutosha kufanya usajili kwa ajili ya msimu ujao na michuano ya UEFA.
Rekodi za Rodgers katika klabu ya LIVERPOOL
Ameongoza mechi 97, ameshinda mechi 54, sare 21 na kupoteza mechi 22 .
Amefunga magoli 206 na kufungwa magoli 118 na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa ni (+88) 
Asilimia ya ushindi ni 55.67 
Mmiliki John Henry na mwenyekiti wa klabu Tom Werner kwa pamoja wamesema: 
"Tuna bahati ya kuongozwa na mtu mwenye kipaji kikubwa katika klabu yetu na tumeweza kuonesha kiwango cha juu na katika yeye tumejenga imani yetu na tutafanikiwa maono yetu". 
"Brendan yuko katika mioyo yetu, kama wamiliki, tunajitahidi kufanikiwa uwanjani. Msimu huu umempa imani kila mmoja kuwa tunaweza kuleta mafanikio Liverpool na tunajitahidi kufanya kazi pamoja ili kufanikisha hilo".
"Wachezaji na mashabiki wameweka wazi jinsi ambavyo Brendan ni muhimu katika mafanikio yetu, hivyo tumeamua kumwamini zaidi na kumpata mkataba mrefu zaidi ambao utamfurahisha kila mmoja wetu".

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI