Saturday, April 5, 2014

WATATU WAFARIKI KWA KUFUNIKWA NA KIFUSI BUNJU

Shughuli ya uokoaji ikiendelea.
Watu Watatu wamekutwa na tukio la kufukiwa na kifusi maeneo ya machimbo ya kifusi huko Bunju , watu hao walikuwa wakichimba kwa bahati mabaya udongo ukamong'onyoka na kuwafukia, wananchi mbali mbali walijitokeza na kusaidia zoezi la uokoaji kwa bahati mbaya wote walipatwa wakiwa wameshafariki 
Watu hao watatu waliofahamika kwa majina ya Msagala, Jacob na Mhando wakazi wa Bunju jijini Dar es Salaam mchana huu wamefariki dunia..
Waokoaji baada ya kugundua mwili ulipo.
Wasamaria wema wakienda kuuhifadhi mwili. Walio fariki imefahamika ni bwana Msagala, Jacob na Mwando wote ni wakazi wa Bunju

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI