Friday, April 11, 2014

RAY C FOUNDATION! IMEKAA POA HII





Wengi wamefarijika na kuingiwa na imani kwa kile alichokianzisha mwanadada huyu ambaye amefanya vizuri sana katika soko la muziki wa kizazi kipya katika miaka ya nyuma...
Hakutetereka pale alipogundua ameyumba na kuamua kufanya maendeleo chanya baada ya kugundua kile kilichomuangusha.
Ray C, ameweza kusimama na kubadilisha maisha yake, nasio maisha yake tu bali mpaka maisha ya wengine walioadhurika na madawa ya kulevya ambapo kwa sasa ameanzisha organization yake itakayokuwa inawasaidia waathirika wa madawa ya kulevya 
Hivi karibuni amekuwa akitupia picha kadha wa kadha katika mitandao mbali mbali zinazoelezea baadhi ya vitu atakavyokuwa akivifanya kuwasaidia waathirika wa madawa ya kulevya.
 
Kwa wale wote ambao wangependa kupata huduma ya mwanadada huyu na foundation yake, ama kama una ndugu alieathirika na madawa watafute Ray C foundation wana ofisi zao Mwananyamala...
Hii ni picha alipokuwa anachukua dawa.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI