Thursday, April 17, 2014

JENNIFER LAWRENCE - ''MWANANGU AMENIBADILISHA KWA KIASI KIKUBWA''

ALIYEKUWA muigizaji katika mfulizo wa mchezo wa kuigiza wa Ghost Whisperer Jennifer Love Hewitt amekuwa katika kiwanda cha burudani kwa miaka mingi sasa na bado anaonekana kuwa ni miongoni mwa wanadada wazuri na wenye mvuto unapomuangalia.
Wanaume wengi wamekuwa wakitamani kuwa naye kimapenzi lakini cha kushangaza ni kuwa mwanadada huyu hana mchechetowa kutaka makuu na hatimaye kuamua kutulia na kujenga maisha yake akiwa na mumewe ambaye alikuwa muigizaji msaidizi katika mfululizo wa vipindi wa Client list, Brian Hallisay ambapo mfulizo huo (Series) ulikuwa ukionyeshwa kupitia luninga mbalimbali nchini Marekani.
Jennifer Love Hewitt akiwa na mumewe Brian Hallisay
Jennifer Love Hewitt alijifungua mtoto mzuri wa kike mwishoni mwa mwaka uliopita, hivi sasa ni kama miezi kadhaa imepita baada ya kujifungua mtoto huyo anaonekana ni mwenye nguvu na kurudi katika hali yake ya zamani kabla ya kujifungua.
Jennifer kipindi akiwa na ujauzito.
Chanzo kimoja cha habari nchini Marekani kinaarifu kuwa Jennifer amekuwa akiongelea kuhusu kupata mtoto aliyemuita Autumn kwa muda mrefu na hatimaye baada ya kujifungua akasema yake ya moyoni kuwa hivi sasa anajiona kuwa ni mtu ambaye moyo wake una amani na upendo umeongezeka sana na amekuwa akimpenda mwanae na anafurahi sana kuwa mama wa mtoto huyo.

Love Hewitt alisema, "Nahisi upend umeongezeka moyoni mwangu kea kiasi kikubwa sana, pia najisikia amani kila muds nimuonapo mwanangu, najisikia poa sana, sipati usingizi kith ambacho nafurahia pia'' Mwanadada hutu maarufu pia akamuongelea mumewe Brian Hallisay, kuwa, "Yupo poa sana, anajali. Muda mwingine ananiona kama mtu fulani nilliyechanganyikiwa, na ilikuwa zaidi kipindi kile cha mwanzo tulipofika nyumbani na mtoto wetu, akawa ananiuliza, 'Unaonekana kama umechanganyikiwa kidogo.' mi nikawa najibu, sawa tutaliongelea hilo baadae."

Kwa upande mwingine, muigizaji huyu kwa sasa amekuwa kimya kidogo katika masuala mazima ya uigizaji, na huenda hili limesababishwa na usitishwaji wa mfululizo wa The Client List, ambapo mfululizo huu (series) ulisimamishwa na kutooneshwa tena katika luninga nchini marekani, kitu ambacho Jennifer Love Hewitt na mumewe Brian Hallisay kiliwauma sana ambapo katika hili, wawili hawa walicheza kama wahusika wakuu, japo kuna uwezekano mkubwa kwa Jennifer kuonekana katika filamu itakayokuja ya Memories Are Made of This.

Angalia picha zaidi za Jennifer hapa!




































0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI