Thursday, April 10, 2014

MH:MWIGULU NCHEMBA ATIMIZA AHADI YA MAJI JIMBONI KWAKE,WAZIRI WA MAJI AMUAHIDI KUSAMBAZA MAJI VIJIJI VINGI ZAIDI

Mh: Waziri wa Maji Prof.Maghembe akiwa ameambatana na Mbunge wa Iramba Mh:Mwigulu Nchemba wakitoka kwenye Tanki Kubwa la Kutunzia maji ndani ya Kijiji cha Nang'uli.
Waziri wa Maji Mh:Maghembe akizindua Mradi Mkubwa wa Maji Kijiji cha Nang'uli Jimbo la Iramba hii leo,Kulia ni Mh:Mwigulu Nchemba akishuhudia tendo kubwa la Maendeleo ndani ya Jimbo lake.
Hatimaye Wananchi wa Kijiji cha Nang'uli na Vijiji Vya Jilani wamepata Mkombozi wa Maji,Mh:Mwigulu Nchemba akimtwisha Ndoo Mama wa Kijijini hapo kuashiria Wamepata Mkombozi wa Maji.
Wananchi wakiwa na Furaha mara baada ya Kukabidhiwa Mradi wa Maji Kijiji cha Nang'uli hii leo.Wananchi wameunda Uongozi wao unaosimamia Uuzaji wa Maji kwenye Chanzo hiki, Ndoo Moja inauzwa Sh.25 tu.Mh:Mwigulu Nchemba akipokelewa na Wananchi wa Kata ya Kinapanda.Wananchi wa Kinapanda wakifuatilia Mkutano kuhusu Maji yatakavyoanza kupatikana Mapema kabla ya Mwaka huu Kuisha.
Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Kata ya Kinapanda kuwaeleza namna anavyoanza kutimiza ahadi yake ya Maji kwenye Kata hiyo,Mh:Mwigulu Nchemba amemleta Mh:Waziri wa Maji kwaajili ya Kutoa kauli yake kuhusu hatma ya Maji ndani ya Kata ya Kinampanda.Waziri Maghembe ameahidi kuwa Kufikia Mwezi wa 12 Mwaka huu,Makao makuu ya Kata ya Kinampanda yatakuwa na Maji ya Kutosha na Wataanza Kusambaza Maji vijiji vya Jilani.Mh:Maghembe akisalimiana na Wananchi wa Ulemo-Iramba wakati akiwasili kwenye Mkutano wa Kuzungumza nao kuhusiana na Upatikanaji wa Maji ndani ya Kata yao na namna Serikali Ilivyojipanga kusambaza Maji Vijijini.
Viongozi wakibadilishana Mawazo,Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mh:Yahya Nawanda,Katikati ni Waziri wa Maji Mh:Maghembe na Mwisho Kulia ni Mh:Mwigulu Nchemba Naibu Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Iramba.
Mh:Mwigulu Nchemba akimshukuru sana Waziri wa Maji kwa Kufanikisha Miradi ya Maji katika Jimbo lake hasa Kata ya Ulemo,Kinampanda,Kiomboi,Ndago na Kijiji cha Nang'uli.
Waziri wa Maji Prof,Maghembe akizungumza na Wananchi wa Ulemo kuhusiana na Utekelezaji wa Mradi wa Maji ndani ya Kata yao.Waziri ameahidi kuwa Serikali imetenga zaidi ya Sh.800 Milioni kwaajili ya Kusambaza Maji kata ya Ulemo.Zoezi hilo limekabidhiwa kwa Mhandisi wa Mkoa/Wilaya na Ofisi ya Mkurugenzi tayari kwaajili ya Kuanza kutimizwa."Maji safiiiiiiiiiiiiiiii"
Wananchi wa Kijiji cha Nang'uli wakishangilia Kupata Maji ndani ya Kijiji Chao.
WAZIRI wa Maji Mhe. Maghembe amefanya ziara ya Kukagua Maendeleo ya Utekelezaji wa Miradi ya Maji Jimbo la Iramba, Katika hatua hiyo Mh:Maghembe amefungua Rasmi Mradi wa Maji wa Kijiji cha Nang'uli na Kuukabidhi kwa Wananchi Waanze kuutumia.
Mbali na Kufungua Mradi huo, Akiwa ameambatana na Mbunge wa Iramba Mh:Mwigulu Nchemba, Prof Maghembe amezungumza na Wananchi wa Kata ya Kinampanda na Ulemo kuhusu Mpango wa Kusambaza Maji ndani ya Vijiji vya Kata hizo pia Kuchimba Visima Vikubwa vya Maji ilikuwezesha Upatikanaji wa Maji ya Uhakika kwa Wananchi.
Maghembe amesema "Serikali imetenga Fedha zaidi ya Milioni 80 kwa Kijiji cha Uleo kwaajili ya Kusambaza Maji,Pia Imetenga fedha kwaajili ya Kuchimba Kisima Kikubwa kata ya Kinampanda kwaajili ya Kupata Maji mengi na hatimaye yasambazwe Vijiji mbalimbali ndnai ya Kata hiyo, Mh:Maghembe amewasihi Wananchi kuunga mkono Juhudi hizo zinazofanywa na serikali ya CCM, Pia amempigia Chepuo Mh:Mwigulu Nchemba kuwa amekuwa Moja ya Wabunge wanaofuatilia sana Mahitaji ya Wananchi wake hasa Maji.
Mbali na Mh:Maghembe, Mbunge wa Iramba N/Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Kinampanda amesema atahakikisha anatimiza kile alichokiahidi kabla hajakwenda kuomba ridhaa ya kuwaongoza tena wananchi wa Iramba, 
"Niliwaahidi maji hapa,nitahakikisha Maji yanapatikana Kabla ya Mwaka 2014 kumalizika, Nashukuru Waziri ametoa kauli kuwa Fedha zipo kilichobaki ni utekelezaji tu, Mkataba wangu na Nyie Wananchi ni Maendeleo tu, Nikishindwa Kuwaletea Maendeleo ni Kutowatendea haki". Mwigulu.
Wakizungumza kwa Nyakati tofauti Wananchi wa Nang'uli na Ulemo wametoa Pongezi zao za dhati kwa Mbunge wao Mwigulu Nchemba kwa Kuwapelekea Maji, Wamesema Wanaona Kazi anayoifanya kwenye Umeme, Elimu, Afya na sasa amewapelekea Maji,Hivyo hawahitaji Kumpoteza kiongozi huyo kwakuwa ni Mchapakazi sana.
Habari na Maelezo: Sanga Festo

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI