Tuesday, April 1, 2014

MATUKIO YA PICHA ZA WAJUMBE BUNGE MAALUM LA KATIBA KAMATI MBALIMBALI MJINI DODOMA

Mwenyekiti wa Kamati namba tano(5) yaBunge Maalum la Katiba Hamad Rashid Mohamed (katikati) akiongoza mjadala wa Kamati hiyo leo mjini Dodoma wakati wanapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.Mwenyekiti wa Kamati namba kumi na moja(11) Anna Kilango akiongea na waandishi wa habari juu ya mambo yaliyojitokeza katika kikao cha Kamati hiyo wakati wanapitia rasimu ya Katiba mpya.Mwenyekiti wa Kamati namba kumi(10) ya Bunge Maalum la Katiba Paul Kimiti (katikati) akiongoza mjadala wa Kamati hiyo leo mjini Dodoma wakati wanapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Salehe Nassoro Juma akitoa mchango wake leo mjini Dodoma kuhusu muundo wa muungano wakati wa kikao cha Kamati namba nne (4) kilichokuwa kinapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Kamati namba nne (4) wakiwa katika kikao leo mjini Dodoma cha kupitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba kwa ajili ya kuiboresha.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati namba nne (4) ya Bunge Maalum la Katiba Dr. Sira Ubwa Maboya (kushoto) akiongoza mjadala wa Kamati hiyo leo mjini Dodoma wakati wanapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa (kushoto) akijadiliana na Mjumbe mwenzake Selemani Jafo leo mjini Dodoma mara baada ya kikao cha asubuhi cha Kamati namba kumi (10) cha kupitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpyaMjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda(kulia) akitoa mchango wake leo mjini Dodoma wakati wa kikao cha Kamati namba mbili(2) kilichokuwa kinapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya. 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Machano Othman Said akitoa mchango wake leo mjini Dodoma kuhusu muundo wa muungano unaofaa wakati wa kikao cha Kamati namba nne (4) kilichokuwa kinapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Joseph Selethin akitoa mchango wake leo mjini Dodoma kuhusu muundo wa muungano unaofaa wakati wa kikao cha Kamati namba tano (5) kilichokuwa kinapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.Mwenyekiti wa Kamati namba tano (5) Hamad Rashid Mohamed akiongea na waandishi wa habari juu ya mambo yaliyojitokeza katika kikao cha Kamati hiyo wakati wanapitia rasimu ya Katiba mpya.Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba , Kamati namba tano (5)wakiwa katika kikao leo mjini Dodoma cha kupitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba kwa ajili ya kuiboresha.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa (kulia) akisamiliana na wajumbe wenzake leo mjini Dodoma mara baada ya kikao cha asubuhi cha Kamati namba kumi (10) cha kupitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Zendi Mvano Abdallah akitoa mchango wake leo mjini Dodoma kuhusu muundo wa muungano unaofaa wakati wa kikao cha Kamati namba kumi (10) kilichokuwa kinapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI