Saturday, April 12, 2014

KONGAMANO LA BIASHARA NA SIKU YA MDAHALO, 25-26/04/2014 BERLIN, UJERUMANI

KARIBUNI WOTE
Kama mnavyofahamu kuwa siku ya tarehe 26 Aprili, 2014 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatimiza miaka hamsini (50), kwa lugha nyingine ni "Golden Jubilee".
Katika kuadhimisha sherehe hii kubwa na muhimu, Ubalozi umeamua kuandaa Kongamano la Biashara (Investment Forum) kwa siku ya tarehe 25 Aprili, 2014 pamoja na siku ya terehe 26 Aprili, 2014 kuwa siku ya mdahalo (Scholars' day) mjini Berlin, Ujerumani.
Madhumuni makubwa ya Kongamano hili ni kuwatangazia na kuwaonyesha umma wa Wajerumani mafanikio mbalimbali yaliopatikana ndani ya muungano wetu kwa kuwaonyesha fursa tulizonazo za biashara katika nyanja za kilimo, utalii, nishati na madani, viwanda, elimu n.k.
Hivyo, Mhe. Philip S. Marmo, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani ana wakaribisha Watanzania wote na marafiki wa Tanzania wanaoishi nchini Ujerumani na wale wanaoishi kwenye maeneo ya uwakilishi ya Ubalozi kuja kushiriki kwenye Kongamano la Biashara siku ya tarehe 25 Aprili, 2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni kwenye ukumbi wa Logenhaus, Emser Str.12-13, 10719 Berlin, Ujerumani.
Aidha, Mhe. Balozi ana wakaribisha pia kwenye mdahalo siku ya tarehe 26 Aprili, 2014 kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana kwenye ukumbi wa Deutsche Bank, Unter den Linden 13-15, 10117 Berlin, Ujerumani.
Kwa maeleozo zaidi piga simu: +49303030800 au tembelea tovuti: www.tanzania-gov.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI