Tuesday, March 25, 2014

WAFAHAMU WANAOWANIA TUZO ZA KILI 2014

Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) limetangaza rasmi matokeo ya mchakato wa kuwapata wateule rasmi yaani ‘nominees’ wa vipengele 34 vya tuzo za muziki Tanzania. Kabla ya kuanza kutajwa kwa wanaowania tuzo za KTMA 2014, BASATA ilitangaza nyimbo ambazo zimetolewa kwenye kuwania tuzo hizi kutokana na sababu za kimaudhui Uzuri wako ya Jux, Nimevurugwa ya Snura na Tema mate tuwachape Madee.
     
Nyingine ni
WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI
Tubonge ya Jose Chameleone, Nakupenda pia ya Wyre na Alaine, Badilisha ya Jose Chameleone, Kipepeo ya Jaguar, Kiboko changu ya Amani, Weasal na Radio.

WIMBO BORA WA TAARAB
Wasiwasi wako wa Mzee Yusufu, asie kujua hakuthamini Isha na Saida Ramadhani, Nipe stara Rahima Machupa, sitaki shari Leila Rashid, fahari ya mwanamke ya Khadija Kopa, mambo bado Khadija Yusufu, kila muomba Mungu ya Mwanahawa Ally.

WIMBO BORA WA RAGGA/DANCEHALL
Nishai ya Chibwa ft Juru, Sexy Lady ya Dr. Jahson, My sweet ya Jettyman Dizano, feel alright ya Lucky Stone na wine ya Princess Delyla.

WIMBO BORA WA KUSHIRIKISHWA/KUSHIRIKIANA
Muziki gani ya Ney wa Mitego ft Diamond, Joto hasira ya Lady Jaydee ft Prof J, kidela ya Ally Kiba na Abdu Kiba, bila kukunja goti ya MwanaFA, Ay ft J Martins na tupogo ya Ommy Dimpoz ft J Martins.

RAPA BORA WA MWAKA WA BENDI
Kitokololo, Chokoraa, Ferguson, Canal Top na Totoo ze bingwa.

MTUMBUIZAJI BORA WA KIKE WA MUZIKI
Khadija kopa, Vanessa Mdee, Isha Ramadhani, Luiza Mbutu, Catherine (Cindy)

MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA TAARAB
Enrico, Ababuu mwana wa Zanzibar na Bakunde.

MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA (BENDI)
Allan Mapigo, C9, Enrico, Amoroso na Ababuu mwana wa Zanzibar.

WIMBO BORA WA REGGAE
Niwe nawe ya Dabo, hakuna matata ya Lonka, tell me ya Dj Aron ft Fidempha, bado nahitaji ya Chikaka ft Bless P & Lazzy B, Bongo reggae ya Warriors from the east.

WIMBO BORA WENYE VIONJO VYA ASILI YA KITANZANIA 
Kwejaga nyangisha ya Batarokota, Nalonji ya Kumpeneka, bora mchawi Dar bongo massive, tumbo lamsokota ya Ashimba, Aliponji ya Wanakijiji na Agwemwana ya Cocodo african music band.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI