Monday, March 17, 2014

WABUNGE WAMGOMEA JAJI WARIOBA, MWENYEKITI AHAIRISHA BUNGE KWA MUDA

MWENYEKITI wa kudumu wa bunge maalumu la katiba Mh.Samweli Sitta amelazimika kuaihirisha mkutano baada ya wajumbe kupinga uwasilisahwaji wa rasimu ya katiba toka kwa mwenyekiti wa tume ya katiba Jaji Joseph Warioba. 

Hali hiyo imejitokeza mjini Dodoma jioni ya leo baada ya baadhi ya wajumbe kusimama wakitaka muongozo kupinga Jaji Warioba kufanya uwasilishaji kabla ya rais kulihutubia bunge wakidai kuwa hatua hii inakikuka kanuni ya 31 ya bunge maalumu la katiba.

Katika kikao cha kwanza baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa kudumu kuliongoza bunge maalumu la katiba mheshimiwa Samweli Sitta analazimika kuahirisha bunge kutokana na msimamo mkali wa baadhi ya wabunge wakidai kuvunjwa kwa kanuni za bunge maalumu la katiba. 

Licha ya jitihada za kuwatuliza wajumbe katika kumpatia nafasi mwenyekiti wa tume ya katiba Jaji Joseph Warioba, wajumbe wanashikilia msimamo wao wakidai alietakiwa kulihutubia bunge kwanza ni Rais na baadae ndio iwasilishwe Rasimu ya Katiba.

Nje ya bunge wajumbe wamekuwa na maoni tofauti tofauti Kuhusiana na suala hilo wangine wakidai ni sawa huku wengine wakisema si sawa. 

Kuahirishwa kwa bunge hilo kumeacha kitandawili kama wajumbe watakubali uwasilishwaji wa rasimu ya katiba ili bunge kuendelea au mpaka rais Kikwete alihutubie kwanza bunge hilo. 
Kwa hisani ya eddy blog.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI