Wednesday, March 12, 2014

UVAAJI WA NGUO ZISIZOSITIRI MIILI KWA WANAWAKE: JANGA!

Hali hii imeendelea kuwatokea wanawake wengi jijini wakiwa wamevalia mavazi yasiyositiri vizuri miili yao, huku wengi wao wakiishia kuzomewa na kuimbiwa nyimbo ambazo mara nyingi huleta fedhea kwao na watu walio karibu nao.

Mfano unamkuta dada kakatiza maeneo ya kariakoo, Posta au Mwenge na kivazi kifupi amabacho huwafanya vijana wa kiume kuwageuza sehemu ya mzaha kwa kuwaimbia nyimbo mbalimbali na huku wengine wakiwatukana matusi mazito mazito na kuwapa maneno ya kashfa.

Ni muda sasa umefika kwa dada zetu kuwa na uchaguzi wa nguo na kuelewa ni wapi nguo gani zinatakiwa kuvaliwa, kwani mwingine unaweza kumkuta amevaa nguo ambazo ni maalumu kwa kuvaliwa nyakati za usiku.

Soma nyakati

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI