Wednesday, March 26, 2014

SIASA ZA KUPATA KATIBA KATIKA BUNGE MAALUM ZAPAMBA MOTO

UTEUZI wa wajumbe watano watakaoingia kwenye kamati ya uongozi uliofanywa na Mwenyekiti wa bunge maalum la katiba, Bw. Samwel Sitta  umeleta mvutano mkubwa miongoni mwa wajumbe baada ya kuutangaza.

Hata hivyo uteuzi huo utakaoambatana na wenyeviti wengine waliochaguliwa kwenye kamati 12 ulichukuliwa na baadhi ya wajumbe kwa hisia tofauti za kutoaminiana kwa kazi wanayokwenda kuifanya mbele yao ya kuandika katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mjumbe mwingine John Mnyika alisema kamati hiyo itaendelea kulalamikiwa  sio tu kwa kukosa uwiano wa pande mbili za muungano bali hata katika upande mmoja wa muungano kukosa sura kabisa ya uwakilishi jambo  ambalo alisema halieleweki.

Hata hivyo Profesa Lipumba  wa chama cha CUF alikanusha kuwa yeye ni mwenyekiti wa kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi-UKAWA  na kusema kuwa  mwenyekiti wake ni Bw. Freeman Mbowe  wa chama cha CHADEMA. Lipumba alisema katika hali inavyokwenda  katika bunge hilo ni wazi kabisa kwamba hakuna nia njema ya  kupata katiba ya wananchi.

Aidha wajumbe wengine walipinga uteuzi huo ambao una wawakilishi kutoka chama tawala cha CCM na kumshauri mwenyekiti huyo wa bunge kufikiria upya juu ya uteuzi alioufanya bila kuegemea vyama vya kisiasa.

Kwa upande mwingine mmoja wa wajumbe aliyesimama kwa muda mrefu kuomba muongozo wa mwenyekiti bila ya mafanikio Bw. Ezekiel Oluochi amedai kuwa randama ya pili ya rasimu ya katiba, ambayo ndiyo yenye uchambuzi wa kina wa mambo yanayobishaniwa hawana wajumbe wengi wa bunge hilo maalum la katiba.
Chanzo: VOA

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI