Thursday, March 20, 2014

OKWI MCHEZAJI WA YANGA ANAELIPWA PESA NYINGI KULIKO MCHEZAJI YEYOTE TANZANIA


Emmanuel Okwi kwa sasa amevunja rekodi ya kuwa ni mchezaji ghali kuliko mchezaji yeyote nchini Tanzania, na hii ni kwa wachezaji wa kigeni na wachezaji wa ndani, na thamani yake imewafunika hata wachezaji wazawa katika timu yake ya Yanga.

Katika nafasi yake ya ushambuliaji kuna Tegete na Javu lakini kutokana na ujio wake wachezaji hao wamekuwa bechi kama wachezaji wa akiba. 

Swali la wengi ni kuhusu kile wanaYanga walichokuwa wanategemea je kimeanza timia au la? kwani wengi wanamatumaini na mchezaji huyu maridadi kabisa aliyeleta mapinduzi kwa vijana wengi nchini Tanzania.

Wapenzi wa Yanga na viongozi walipo mpokea Okwi kwa mbwembwe.

Okwi akitambulishwa makao makuu ya Yanga Jagwani
Wapenzi wa Yanga wakiwa wameshika jezi yenye jina la Okwi wakifurahia ujio wa mchezaji huyo matata aliyewahi ichezea SIMBA kwa kipindi fulani.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI