
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Hussein Javu, akijiandaa kupiga shuti langoni mwa Tanzania Prisons, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliochezwa jana jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo Yanga ilishinda mabao 5-0. Yanga ilianza kufungua ukurasa wa mabao yake katika Dakika ya 20 kupitia mshambuaji wake Emmanuel Okwi, aliyefunga bao kwa mpira wa adhabu 'Direct Kikck', Dakika ya 35, Tz Prisons walipata penati iliyopigwa na Nahodha wao ambaye alikosa na katika dakika ya 38, Mrisho Ngasa, aliifungia Yanga bao la pili na katika dakika ya 68 Hamis Kiiza, aliwainua tena mashabiki wa Yanga kwa kuandika bao la tatu.
Dakika 78, Yanga ilipata bao la nne kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub Canavaro, huku bao la tano likifungwa tena na Hamis Kiiza katika dakika ya 89.
Pamoja na Yanga kuibuka na ushindi mnono lakini bado Azam Fc wanaendelea kukalia usukani wa Ligi hiyo, baada na wao kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mgambo Shooting, katika mchezo wao uliochezwa jana jioni kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
Kwa sasa Azam wanaongoza Ligi wakiwa na jumla ya Pointi 50 huku Yanga wakiwafuatia wakiwa na Pointi 46, na pia wakiwa na mchezo mmoja mkononi zaidi ya Azam.
Mbio hizi za kuwania ubingwa kwa timu hizi mbili bado ni ngumu kwani kila timu imeshajiweka vizuri kuhakikisha inaibuka na ushindi katika michezo yake yote iliyosalia, na iwapo timu zote zitashinda katika michezo yote iliyobaki, basi Azam Fc watakuwa mabingwa kwa tofauti ya Pointi 1 tu na Yanga.

Simon Msuva (kushoto) akiwahenyesha mabeki wa Tanzania Prisons.

Emmanuel Okwi, akimiliki mpira....

Wachezaji wa Tanzania Prisons, wakipeana moyo ili kurejea kumalizia dakika 45 za kipindi cha pili.

Mrisho Ngassa, akimzunguka kipa wa Tanzania Prisons.

Kipa wa Tanzania Prisons, akiruka kupangua moja ya hatari zilizoelekezwa langoni kwake.

Wachezaji wa Tanzania Prison, wakimlalamikia mwamuzi wa mchezo huo baada ya kuamuru mkwaju wa penati






0 comments:
Post a Comment