Na Hilali Ruhundwa
TUME ya mchakato wa mabadiliko ya katiba mpya nchini
imeshauriwa kutumia ripoti ya katiba na sharia ya chama cha sharia cha
wanawake nchini ili kuzingatia masuala ya jinsia na haki zake.
Chama
cha sheria cha wanawake Tanzania, kimeitaka tume ya mabadiliko ya katiba
nchini, kuhakikisha kuwa inawashirikisha wananchi wote hasa wa
vijijini, ili kutoa maoni ya ulingano wa kijinsia katika katiba hiyo.
Hayo
yamebainishwa na mratibu wa jinsia wa chama cha sheria cha wanawake
nchini Debora Mushi, wakati wa uzinduzi wa ripoti ya katiba na sheria ya
chama hicho, na kusema kuwa miongoni mwa mambo yaliyomo katika ripoti
hiyo, yanaweza kutumiwa na tume ya mabadiliko ya katiba mpya, ili kutoa
katiba yenye ulingano wa kijinsia.
Ameongeza kuwa haki zote za
makundi hayo, ni muhimu ziingizwe ktk katiba mpya, ikiwemo haki za
wanawake na makundi mbalimbali, sanjari na kuweka ukrasa maalum,
unaoonesha utekelezaj wake.
Jamhuri ya muungano wa Tanzania, ipo
katika ukusanyaji wa maoni ya wananchi, kuhusu mchakato wa uundwaji wa
katiba mpya, ambapo hivi karibuni, waziri mkuu wa Tanzania Mizengo
Kayanza Peter Pinda, amesema kuwa zoezi hilo linaendelea vizuri, na
kwamba kufikia mwaka 2014, itapatikana katiba mpya iliyotokana na
wananchi.
Friday, November 9, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ZILIZOSOMWA ZAIDI
-
MTANDAO wa Swahili Worldplanet unaarifu kuwa, picha chafu zinazodaiwa kuwa za star wa filamu nchini Shamsa Ford na mbunge wa Chadema, ...
-
IDADI ya watu wanaoendelea kutajwa kupata tiba ya Ebola, imezidi kuongezeka, leo pia shirika la utangazaji Sky News wameripoti kuhus...
-
MCHEZAJI Cristiano Ronaldo amesaini mkataba mpya na klabu yake ya Real Madrid utakaomalizika Mwaka 2021, amesema anaweza kuendelea kuc...
-
1. NISHA JABU 2. FLAVIANA MATATA 3. NELLY KAMWELU 4. JOKATE MWEGELO 5. NANCY SUMBELARI 6. BELINA MGENI 7. VANESSA M...






0 comments:
Post a Comment