NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Friday, January 11, 2013

JE UNGEPENDA UPATE KALENDAR YAKO MWENYEWE KAMA HII?

Ni kati yakalenda za mwaka 2013 ya mrembo Mary, Ukitaka kama hii yenye picha yako utaipata... Zinapatikana kwa gharama nafuu ya sh 4000 tu.. Wasiliana nasi kwa namba 0715771212 au 0715431721

SERIKALI YALIFUFUA SHIRIKA LA RELI

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete (yumo garini kushoto) akikagua sehemu ya kutua na kupaa ndege ya uwanja wa Tabora  Januari 10, 2013 mara baada ya kuzindua rasmi ujenzi wake
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mhe Radhia Msuya mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataikfa wa Julius Nyerere jijini
Dar es salaam akitokea mkoani Tabora alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku tano kukagua shughuli za maendeleo na kuzindua miradi mbalimbali
(Picha: Ikulu)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
SERIKALI imetangaza hatua kubwa na kabambe za kufufua usafiri wa abiria na mizigo,  ikiwa ni pamoja na ununuzi wa mabehewa na injini za treni, katika hatua kubwa za aina yake kuchukuliwa na Serikali kwa muda mrefu katika kurekebisha usafiri wa treni nchini.
Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa Harrison George Mwakyembe ametangaza hatua hizo leo, Alhamisi, Januari 10, 2013, wakati alipokuwa anamkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuweka jiwe la msingi kwenye ukarabati mkubwa wa Uwanja wa Ndege wa Tabora ikiwa ni tukio la mwisho la ziara yenye mafanikio makubwa ya siku tano ya Rais Kikwete katika Mkoa wa Tabora.
Mheshimiwa Mwakyembe amemwambia Rais Kikwete na mamia kwa mamia ya wananchi waliohudhuria sherehe ya uwekaji jiwe hilo la msingi kwenye Uwanja huo kuwa Wizara yake imeanza kubadilisha reli nyepesi, iliyochakaa na yenye uzito mdogo kwa Reli ya Kati.
Amesema kuwa kwa kupitia mashirika yake ya RAHCO na Shirika la Reli Tanzania (TRL) Serikali itafanya marekebisho hayo makubwa njia mzima ya Reli ya kati na kuwa mafundi wa mashirika hayo tayari wamefika Mkoa wa Morogoro.
Waziri Mwakyembe amemwambia Rais Kikwete kuwa Serikali kupitia Wizara yake na mashirika yake hayo, imeagiza mabehewa mapya ya mizigo 274, imeagiza mabehewa mapya ya abiria 22, imeagiza mabehewa mapya ya kubebea kokoto 25 na pia imeagiza mabehewa ya breki (brake vans) 34 na tayari malipo ya awali yamefanyika.
Katika namna inayothibitisha dhamira ya Serikali kurekebisha hali ya usafiri wa reli nchini, Mheshimiwa Mwakyembe pia amewaambia wananchi kuwa Wizara yake pia imeagiza crane mpya na kubwa ya kubebea mizigo yenye uzito unaofikia kilo 100.
Kuhusu injini za treni, Waziri Mwakyembe amemwambia Rais Kikwete kuwa zabuni kwa ajili ya kutengeneza upya (re-manufacturing) injini nane za treni imetolewa ili utengenezaji huo ufanyike, iwe ni ndani ama nje ya nchi.
Pia Waziri amesema kuwa oda imetolewa kwa ajili ya utengenezaji wa injini mpya 13 za treni ambazo malipo yake yatafanyika katika mwaka ujao wa fedha hata kama utengenezaji wa injini hizo utaanza.
Aidha, Waziri amesema kuwa Wizara kupitia mashirika yake hayo mawili imeagiza spea za kutosha kuweza kufanya ukarabati mkubwa wa injini tano kwenye karakana zilizoko hapa nchini.
“Mheshimiwa Rais, kwa hesabu nyepesi tu ni kwamba katika kipindi kifupi tutaweza kuwa na injini kiasi cha 26 ambazo zitarudisha uhai wa usafiri wetu wa reli kwa kiasi kikubwa sana,” Waziri Mwakyembe amemwambia Rais Kikwete.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

10 Januari, 2013

DARAJA LA MBUTU, IGUNGA KITENDAWILI KILICHOTEGULIWA NA RAIS JAKAYA KIKWETE HIVI KARIBUNI

Thursday, January 10, 2013

WASANII WA FILAMU WALIVYONOGESHA UZINDUZI WA KAMPENI YA KILIMO KWANZA KATA YA KWADELO, KONDOA

 Wasanii wa filamu, kutoka kushoto; Jacob Steven 'J B',  Vicent Kigosi 'Ray', Irene Uwoya, Wema Sepetu na Single Mtambalike 'Rich Rich' walipowasili Kwadelo kwa ajili ya kushiri uzinduzi huo wa kampeni ya Kilimo Kwanza kwa vijana wa Kata hiyo.
 Wazee wa Kwadelo wakati wakisubiri kuwasili kwa diwani wao pamoja wasanii hao
 Baadhi ya akinamama wa Kwadelo waliohudhuria hafla hiyo
 Ray akipozi picha na wazee wa Kwadelo
 Kariati akiwa na wasanii hao kwenye trekta kabla ya uzinduzi wa kampeni hiyo
 Wema Sepetu akiungurumisha trekta ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa kampeni hiyo. Wapili Kulia ni Omary Kariati
 Uwoya naye akilijaribu trekta kwenye uzinduzi huo
KWADELO HOYEEEEEE! JB akihamasisha wakati wakiwa kwenye trekta la kilimo katika uzinduzi huo
 Treka likionyesha mfano wa ulimaji wa kisasa kwenye shamba la shule ya sekondari ya Kwadelo wakati wa uzinduzi huo
 KITUKO: Panzi! Panzi! Panzi!, Wema Sepetu (shati ya kijani) akifunika uso wake kwa kipochi chake, huku akipiga kelele na kujiingiza katika kundi la wazee,  kwa sababu ya kuogopa panzi aliyemdandia wakati wa shughuli za uzinduzi huo shambani.
 J B na Wema wakila mapozi shambani wakati wakienda sehemu ya uzinduzi
 Wema akitangaza kuzindua kampeni hiyo
 BAADAYE: Wasanii hao wakimkabidhi sh. 500,000 mmoja wa wananchi wa Kwadelo walioathirika na mafuriko. Kwa mujibu wa Diwani Kariati (wapili kushoto), fedha hizo zimetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Meembe ambaye ni mzee wa heshima wa kata hiyo.
 Diwani Kariati akikagua maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko katika moja ya vijiji vya Kata ya Kwadelo, kufuatia mvua zoinazoendelea katika maeneo mbalimbali nchini
 Kariati akionyeshwa maeneo yaliyoathirika
Wazee wakiomba dua ya kheri baada ya shuguli za uzindizi wa Kampnei ya kilimo kwanza na kukagua maeneo ya walioathiriwa na mafuriko: Picha  na Bashir Nkoromo.

SERIKALI YAPANIA KUFUFUA RELI TANZANIA

Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli (kulia)  na Waziri wa  Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe wakiongea wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Tabora leo Januari 10, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mhe Radhia Msuya mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataikfa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea mkoani Tabora alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku tano kukagua shughuli za maendeleo na kuzindua miradi mbalimbali
 (PICHA NA IKULU)
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
SERIKALI imetangaza hatua kubwa na kabambe za kufufua usafiri wa abiria na mizigo,  ikiwa ni pamoja na ununuzi wa mabehewa na injini za treni, katika hatua kubwa za aina yake kuchukuliwa na Serikali kwa muda mrefu katika kurekebisha usafiri wa treni nchini.

Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa Harrison George Mwakyembe ametangaza hatua hizo leo, Alhamisi, Januari 10, 2013, wakati alipokuwa anamkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuweka jiwe la msingi kwenye ukarabati mkubwa wa Uwanja wa Ndege wa Tabora ikiwa ni tukio la mwisho la ziara yenye mafanikio makubwa ya siku tano ya Rais Kikwete katika Mkoa wa Tabora.

Mheshimiwa Mwakyembe amemwambia Rais Kikwete na mamia kwa mamia ya wananchi waliohudhuria sherehe ya uwekaji jiwe hilo la msingi kwenye Uwanja huo kuwa Wizara yake imeanza kubadilisha reli nyepesi, iliyochakaa na yenye uzito mdogo kwa Reli ya Kati.

Amesema kuwa kwa kupitia mashirika yake ya RAHCO na Shirika la Reli Tanzania (TRL) Serikali itafanya marekebisho hayo makubwa njia mzima ya Reli ya kati na kuwa mafundi wa mashirika hayo tayari wamefika Mkoa wa Morogoro.

Waziri Mwakyembe amemwambia Rais Kikwete kuwa Serikali kupitia Wizara yake na mashirika yake hayo, imeagiza mabehewa mapya ya mizigo 274, imeagiza mabehewa mapya ya abiria 22, imeagiza mabehewa mapya ya kubebea kokoto 25 na pia imeagiza mabehewa ya breki (brake vans) 34 na tayari malipo ya awali yamefanyika.

Katika namna inayothibitisha dhamira ya Serikali kurekebisha hali ya usafiri wa reli nchini, Mheshimiwa Mwakyembe pia amewaambia wananchi kuwa Wizara yake pia imeagiza crane mpya na kubwa ya kubebea mizigo yenye uzito unaofikia kilo 100.

Kuhusu injini za treni, Waziri Mwakyembe amemwambia Rais Kikwete kuwa zabuni kwa ajili ya kutengeneza upya (re-manufacturing) injini nane za treni imetolewa ili utengenezaji huo ufanyike, iwe ni ndani ama nje ya nchi.

Pia Waziri amesema kuwa oda imetolewa kwa ajili ya utengenezaji wa injini mpya 13 za treni ambazo malipo yake yatafanyika katika mwaka ujao wa fedha hata kama utengenezaji wa injini hizo utaanza.

Aidha, Waziri amesema kuwa Wizara kupitia mashirika yake hayo mawili imeagiza spea za kutosha kuweza kufanya ukarabati mkubwa wa injini tano kwenye karakana zilizoko hapa nchini.
“Mheshimiwa Rais, kwa hesabu nyepesi tu ni kwamba katika kipindi kifupi tutaweza kuwa na injini kiasi cha 26 ambazo zitarudisha uhai wa usafiri wetu wa reli kwa kiasi kikubwa sana,”Waziri Mwakyembe amemwambia Rais Kikwete.
 Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
 10 Januari, 2013

Monday, January 7, 2013

ZIARA YA KIKWETE IGUNGA ILIVYOTIKISA!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutumia mamia ya wananchi wa Igunga katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika uwanja wa Barafu mjini Igunga baada ya kuzindua ujenzi wa daraja la Ndutu pamoja na mradi mkubwa wa maji utaohudumia asilimia 70 ya wakazi wa Igunga.
Mamia ya wananchi wakiwa wamefurika katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika uwanja wa Barafu mjini Igunga baada ya kuzindua ujenzi wa daraja la Ndutu pamoja na mradi mkubwa wa maji utaohudumia asilimia 70 ya wakazi wa Igunga.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia wananchi mbalimbali waliojitokeza katika mkutano wa hadhara mjini Igunga leo. 
Wananchi wa Igunga wakipunga mikono wakati Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akiwahutubua katika viwanja vya Barafu mjini Igunga leo. (Picha na Ikulu)

Sunday, January 6, 2013

NGOMA MPYA YA R.O.M.A ft STORY - 2030.

STORY NYUMA YA PAZIA,,, KUTOKA KWA ROMA MWENYEWE...!

Habari mabibi na mabwana!! poleni na mihangaiko ya siku!! naam ijumaa iliyopita nilitoa kibao changu maridhawa kipya kabisa kinaitwa 2030!!! na nilikiachia kwa radio stations zote nchini kadri ya uwezo wangu/wetu, though kutokana na mawasiliano ni ngumu kufikia radio zote kwa wakati, ila nyingi ziliupata!!! lakini niliweka utaratibu fulani kwa watakaohitaji kuupata huo wimbo 2030 mbali na radio basi wataupata kwa kussuport kuununua on line kwa tsh 3000/=!!nilishatangaza sana mnafahamu!!ilikuwa ni trial ya kuona nani ana love ya kussuport na nani hana kupitia njia zilizowekwa na sio njia nyingine. zoezi limeenda kwa challenge nyingi sana asante wote waliossuport katika hili, pia asante kwa wale walioliharibu zoezi hili maana imenifanya nimtambue hu z real na hu z fake!!! imeniuma kuona wapo wasanii wanafanya biashara kama hii wanauza mix tapes, album,tisherts zikiwa zote ni movements za kuleta changes ktk mziki wetu, then hao hao wanakuwa mstari wa mbele kupinga hii movement yangu halafu bila sababu yani dah SHALL WE MAKE IT????? nway lilikuwa ni zoezi lililopangwa kufanyika kwa week moja 1 tu ili kuona na kufanya tathmini kuwa yanawezekana haya?najua wengi wanasubiri feed back ya mauzo haya haikuwa nzuri sana kwa wingi wa nyomi nililokuwa nalo, lakini pia haikuwa mbaya maana ni mageni haya..kwa siku 7 za mauzo ilikuwa kila siku wananunua watu wasiopungua 50!! so unaweza ona hapo kuwa yanawezekana haya tukiyawekea mkazo...ILA SIAMINI KAMA KILA MSANII ANAWEZA FANYA, INATEGEMEA NA NGUVU YA MSANII HUSIKA NA KIBAO ALICHOKITOA..(IFIKIE KIPINDI TUONGEE UKWELI TUU!!)wengi wameanza kufanya biashara kupitia nyimbo hii na inawanufaisha wao, wengi wamerecord radio wimbo huu kitu kilichopelekea kukosa quality na bado wanauzia wengine so wanapewa kitu kisicho na quality, pia wengi wanakwazika na mengi yaliyoongelewa ndani ya wimbo huu na wanakosa majibu maana wanakosa fursa ya kuusikia mara kwa mara kwasababu hawajaunga mkono hii movement!! au pengine imekuwa ni njia ngumu kwao kuupata, basi kwa wale waliossuport kwa kuinunua nawashukuru sana na mungu awaongezee mlipopungukiwa, najua litatokea hili la kujiona wanyonge kuwa ROMA amechukua fedha zetu na kisha ameachia bure, mi naamini ukiwa muelewa na ukiona nilichokisema hapo juu hautakwazika as long umeonyesha lav yako kwa msanii unayemfeel, samahani sana kama nitakuwa nimekukosea,nimefanya hivi kama kuanzisha hiki kitu na naamini wengine watafatia na kukiboresha zaidi!!LAZIMA APOTEE MMOJA ILI KUMI WAISHI VEMA NDIPO YATAPATIKANA MAENDELEO!! AM SO SORRY!!! So leo wiki imetimia na wimbo umetoka rasmi na hauuzwi tena kama ilivyotangazwa awali. unapatikana bure kwenye net, download via access yoyote utakayoiona!! nimeutoa rasmi kwenye blogs mbali mbali ANZIA NA YA DJ CHOKA, na nyinginezo!! Na version iliyopita kuchezwa radio ni version ya ROMA ile beat yake iliyochangamka ambayo ni version ya 1 ambayo ndiyo ilikuwa ya kwanza kutambulishwa ijumaa pale clouds fm radio. kwa maswali zaidi tutameet kwenye mainterviewz huko maradioni na tutawekana sawa!! samahanini kwa wote niliowakwaza, asanteni kwa wote mliossuport!! ROMA 2030 INAPATIKANA FREE SASA!!! 

Anakwenda kwa jina la STORY ndiye aliyeimba CHORUS ya nyimbo mpya ya ROMA - 2030 (ILE SAUTI YA KITOTO)

ZILIZOSOMWA ZAIDI