NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Tuesday, July 12, 2016

KITUO CHA DK. MWAKA CHAFUTIWA USAJILI, WENGINE KUSIMAMISHWA MIEZI 6 NA KUPEWA ONYO KALI

BARAZA la Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini, limekifutia usajili wake wa kutoa huduma za kitabu, Kituo cha Tiba Asilia cha ForePlan Kliniki kilichopo Ilala Bungoni jijini Dar es salaam, kinachomilikiwa na Dkt. Juma Mwaka maarufu kama Dkt. Mwaka, kwa madai kuwa kimekiuka taratibu za kitabu za tiba mbadala.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dkt. Edmund Kayombo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ukumbi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Akizungumza jijini Dar es salaam leo katika Mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dk. Edmund Kayombo amesema kuwa kufutiwa kibali cha Dk. Mwaka kunatokana na sababu nyingi ambazo amekuwa akikiuka licha ya kupewa maonyo na barua juu ya utoaji huduma zake.

Amesema sababu nyingine ni kuwa katika matangazo yake amesema anatoa tiba za kisasa wakati hiyo elimu hana ya kufanya huo.

Wengine waliofutiwa usajili ni Fadhaget Sanitarium kinachoendeshwa na Tabibu Fadhili Kabujanja pamoja na Mandai Herbal Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Abdallah Mandai

Hata hivyo limetoa adhabu mbalimbali kwa kituo cha Aman Herbal Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Esbon Baroshigwa, na Tabibu Castory Ndulu wa Kituo cha Ndulu Herbal Clinic wamepewa barua ya onyo.


Aidha wengine wamesimashwa kwa miezi sita ambao ni Tabibu John Lupimo wa Lupimo Suntarium Herbal Clinic pamoja na Tabibu Simon Rusigwa wa Sigwa Herbal Clinic.

WAKURUGENZI WATENDAJI WA HALMASHAURI, MIJI, MANISPAA NA MAJIJI 185 WALA VIAPO VYA MAADILI IKULU LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri, Miji, Manidpaa na Majiji 185 kabla ya hawajakula kiapo cha maadili ya viongozi leo Ikulu jijini Dar es salaam. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Mkutano ulioitishwa  na Rais John Magufuli kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote za wilaya na baadhi ya Wakuu wa  wilaya  ikulu jijini Dar es salaam Julai 12, 2016.
Sehemu ya Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri, Miji, Manidpaa na Majiji 185 wakipata maelezo ya awali kabla ya kula kiapo cha maadili ya viongozi leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri, Miji, Manispaa na Majiji 185 wakila kiapo cha maadili ya viongozi leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Wakuu wa wilaya za Kongwa Mhe deo Ndejembi (kushoto), Siriel Shaidi Mchembe (DC Gairo) na Mhe. Geoffrey Idelphonce Mwambe (DC Manyoni) wa kila kiapo cha maadili ya viongozi leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukosa kufanya hivyo na wenzao wiki iliyopita.
#Picha na Ikulu

BABY FUTURE AANZA KUMUITA MUME WA CIARA ‘BABA’ *VIDEO*

13652111_220707744990138_1412425769_n
Hivi karibuni Ciara alifunga ndoa na mchumba wake Russell Wilson nchini Uingereza. Na sasa mtoto aliyezaa na rapper Future ameanza kumuita Russell ‘Papa’ neno linalomaanisha ‘Baba.’
Video inayomuonesha mtoto huyo akimuita baba yake wa kufikia ‘Papa Russ’ imesambaa mtandaoni. Mtoto huyo anaonekana akimuomba busu Russell na yeye kumjibu ‘You’re so sweet.’
Hivi karibuni mahakama iliamua Ciara na Future wawe na haki sawa za kumleta mtoto wao aitwaye Future.
Wilson na Ciara walifunga ndoa wiki iliyopita.

Monday, July 11, 2016

COUPLE 10 ZA MASTAA WABURUDISHAJI ZENYE NGUVU ZAIDI TANZANIA – 2016 *PICHAZ*

13395089_214032905662116_1444251759_n
Tanzania imebarikiwa kuwa na tasnia ya burudani yenye watu wenye nguvu sana.
Lakini nguvu yao huwa maradufu pale wakiwa na uhusiano wa kimapenzi na mastaa wenzao. Ninakuletea orodha ya couple 10 za mastaa wa Tanzania zenye nguvu zaidi kwa sasa. Nguvu zao zipo kwenye lundo la mashabiki walionao, ushawishi wao, utajiri wao na wafuasi walionao kwenye mitandao ya kijamii. Wengi ni kutokana na jinsi walivyodumu kwa muda mrefu, kutumia brand zao kwa pamoja kujikuza na mambo mengine kibao.
1. Diamond Platnumz na Zari the Bosslady
13395089_214032905662116_1444251759_n

Himaya ya Diamond yenye utajiri unaokadiriwa kuwa zaidi ya shilingi bilioni 8 ina nguvu isiyoelezeka pale inapoungana na mwanamke aliyeachiwa utajiri mkubwa na ex wake na kujitengenezea himaya yake mwenyewe pia. Wanakaribia kufikisha miaka miwili sasa tangu wawe pamoja na ukikumbuka walivyoanza kwa kujiita ‘project’ hakuna aliyewahi kudhani kama wangeendelea kudunda hadi leo.
Sasa hivi ni wazazi wa mtoto wao mwenye miezi 11, Tiffah. Hii ni couple inayozungumzwa zaidi Afrika Mashariki, isiyokauka kwenye vichwa vya habari vya magazeti ya udaku kila iitwapo leo. Ni couple inayojadiliwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii na lundo la wafuasi walio nyuma yao tayari kwa kumshambulia yeyote anaye hatarisha uwepo wake, linatisha. Kwa pamoja wana wafuasi kwenye Instagram zaidi ya milioni 4.2 huku mtoto wao akiwaongezea wengine 700k na kuwa na takriban milioni 5.
Pamoja na hivyo, hii ni couple isiyokaukiwa misukosuko na skendo kibao zikiwemo za Diamond kuwahi kudaiwa kuchepuka na mrembo wa video ya Kwetu ya Raymond hadi tetesi kuwa Zari hana maelewano mazuri na ndugu za mchumba wake. Zari pia amekuwa akiwekwa kitimoto kwa kuendelea kuwa na mawasiliano na ex wake, Ivan, kitu ambacho hakiepukiki sababu wana watoto watatu wa kiume waliozaa pamoja.
Pamoja na hivyo, bado wameendelea kuonesha kutoteteleka na dhoruba hizo na mashua yao inaendelea kukata mawimbi baharini na huenda Tiffah akaja kupata mdogo wake, huku pia uwezekano wa kufunga pingu za maisha siku za usoni ukiendelea kuwa mkubwa.

2. Idris Sultan na Wema Sepetu

Wema
Mshindi wa Big Brother Africa aliyegeuka kuwa milionea ndani ya miezi mitatu na Miss Tanzania 2006 na muigizaji maarufu zaidi wa filamu Bongo wanapounda umoja wa kimahaba, matokeo yake ni makubwa. Idris Sultan na Wema Sepetu wana nguvu kubwa ambayo couple pekee iliyo na cheche za kuwazidi ni hiyo ya juu.
Hata hivyo yote yanarudi na kuanzia nyuma tena. Wema alikuwa kwenye uhusiano maarufu na wa muda mrefu na Diamond ambao bahati mbaya pamoja na kuachana, hadi leo harufu za mahaba yao zimeendelea kuwanyemelea na kutengeneza chuki na upendo kwa pamoja.
Idris alijikuta akizidiwa na nguvu ya umaarufu wa uhusiano wao hadi kuapa kutouweka hadharani tena – kitu ambacho kinaonesha ni kigumu kukifanikisha. Wao pia walikaribia kufika kwenye hatua muhimu ya kupata mtoto – mapacha, lakini kwa maneno yao wenyewe, Mungu hakupenda iwe hivyo. Bado suala la Wema kutopata mtoto limeendelea kuwa kidonda kibichi kinachotoneshwa mara nyingi.
Idris na Wema wamepitia majaribu mengi ambayo wakati mwingine huyashindwa kuyahimili na kuachana, lakini hugundua bado wanapendana na kurudiana tena. Kwa mfano kipindi video ya Wema imesambaa mtandaoni akimbusu mwanaume mwingine, iliuvunja moyo wa Idris kiasi cha kuamua kulivua pendo – kwa muda.
Hivi karibuni pia baada ya Wema na Diamond kuonesha kuvunja uhasama wao, Wema kumtumia salamu za siku ya kuzaliwa Bi. Sandra (mama yake Diamond) Idris alitafsiriwa na wengi kujikuta njia panda kwa mtazamo kuwa hapewi heshima anayostahili na mpenziwe. Hata hivyo hakujali na kwa wale waliohudhuria show yao ya Black and Tie, mwishoni mwa wiki, walishuhudia jinsi njia hao walivyokuwa wakitembea kama kumbi kumbi – mapenzi tele.
3. Alikiba na Jokate Mwegelo
KIba
Pamoja na wao wenyewe kuendelea kukwepa kukiri hadharani kuwa ni mtu na mpenzi wake, ni kipofu pekee asiyeweza kutambua pendo zito lilivyowajaa, Alikiba na Jokate Mwegelo. Wamekuwa pamoja kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa kiasi ambacho uhusiano wao sio siri tena katika familia za pande zote mbili – ikiwa ni pamoja na Jokate kutambua na kujali uwepo wa watoto wa Alikiba.
Wamekuwa wakitengeneza headlines nyingi mno kwenye magazeti ya udaku kuhusu uhusiano wao lakini hadi sasa hawataki kuwapa kile mashabiki wao wamekuwa wakikiota kwa muda mrefu – kuuweka uhusiano wao wazi kama couple hizo juu.

Kitendo cha kuficha mahusiano yao si kigeni hata katika maisha yao ya nyuma. Pamoja na kuwahi kuwa na uhusiano na Hasheem Thabeet na kisha Diamond kwa muda mfupi, Jokate hajawahi kupendelea kuweka wazi maisha yake binafsi.
Alikiba pia vivyo hivyo, pamoja na kuwa na watoto watatu hadi sasa, kila mmoja na mama yake, hakuwahi kuwa mtu wa kuwaweka wazi wapenzi wake. Vyovyote ilivyo, mapenzi yao yanaonekana wazi kwa wale waliowahi kubahatika kuwaona wakiwa pamoja na pengine kuna siku wataamua kuuweka rasmi uhusiano wao kama mastaa wengine.
4. Jux na Vanessa Mdee
Jux and Vanessa Mdee
Iliwachukua muda mrefu sana Jux na Vanessa Mdee kukiri kuwa ni wapenzi. In fact, pamoja na kuamua kuuweka wazi, bado si watu wanaofurahia sana mada ya uhusiano wao. Wana takriban miaka miwili sasa tangu waanze kuwa pamoja.
Kuna wakati waliamua kuuweka wazi kidogo uhusiano wao kwa kuweka picha zao wakiwa kwenye mitandao ya kijamii, lakini sasa wameamua kuacha japo kwa walio karibu nao wanafamu jinsi wawili hawa wanavyopendana na kusaidiana katika kazi zao.

Kuna wakati pia Jux alimtumia Vee kwenye video yake lakini pia mara kibao Jux amekuwa karibu na mpenzi wake wakati akishoot video zake SA – mfano wakati akishoot video ya Never Ever.
Nina uhakika kuwa Jux ana ushindani mkubwa kuhakikisha kuwa Vee anaendelea kuwa wake daima na hii ni kutokana na umaarufu alionao Vanessa barani kote huku safari za nje zikiwa hazikauki. Jux pia kwa upande wake anafahamika kwa maisha ya kifahari aliyonayo na hivyo kujitengenezea sumaku inayovutia warembo wengi, achilia mbali maisha yake ya kusafiri mara kwa mara kwenda China masomoni.
Kwa namna yoyote ile, wawili hawa wanaonekana kuendana vyema na nina uhakika bado wana miaka mingi ya kuendelea kuwa pamoja.
5. Master J na Shaa
Master-J
Master J na Shaa walikutana takriban miaka kumi iliyopita. Shaa alikuwa msichana mdogo ambaye damu ya kufanya muziki ilikuwa ikichemka na kushinda shindano la Cocacola Popstars. Master J aliteuliwa kwenda nao Afrika Kusini kama producer wa kundi lililoanzishwa, Wakilisha. Baada ya kurudi, Shaa kwenda tena Marekani kusoma na kundi likavunjika, Shaa alirejea na kuwa chini ya MJ Records.
Sifahamu uhusiano wao kimapenzi ulianza lini lakini wana muda mrefu sana kwa sasa. Uhusiano wao umepitia majaribu mengi pia kuanzia Master J kutengana na mke wake aliyezaa naye watoto watatu warembo wa kike hadi Shaa kulalamikiwa kuwa sababu ya kuvunjika kwa ndoa hiyo. Master J amewahi kukiri mara nyingi kuwa kuvunjika kwa ndoa yake lilikuwa jaribu kubwa zaidi katika maisha yake. Hata hivyo yeye na Shaa waliendelea kuwa madhubuti na hivi karibuni walidai kuwa wana mpango wa hatimaye kufunga ndoa.

6. Barakah Da Prince na Naj

13628138_1240767765933440_485090523_n
Kupanda chati na kufahamika haraka kwa Barakah Da Prince hakujatokana na hits zake tatu pekee – Siachani Nawe, Nivumilie na Siwezi, bali jinsi anavyoitupa karata yake kwenye masuala yahusishayo moyo. Amewahi kuhusishwa kuwa na uhusiano na list ndefu ya mastaa wakiwemo Meninah, Linah, Agnes Masogange, Nisha na hatimaye sasa akiwa na Naj aliyemrasimisha zaidi.
Naj, historia yake yake naye ni ya kipekee. Hakupata jina kupitia hit single yake na Mr Blue ‘Please Don’t Go’ tu bali kwakuwa na uhusiano na rapper huyo aliyemtumia pia kwenye video ya hit single yake, Tabasamu.
Barakah amekuwa mpenzi wake wa kwanza tangu aliporejea kutoka Uingereza alikokuwa masomoni kwa miaka mingi. Kwa sasa penzi la msanii huyo mpya wa Rockstar4000 na Naj limezidi kupamba moto na hawaoni haya kueleza wazi wanavyopendana.
7. Majizzo na Lulu
13557244_171259513288748_1474298025_n
Nilianza kuona dalili za kuwepo uhusiano wa Majizzo na Lulu miezi kadhaa iliyopita wakati wa tuzo za Africa Magic jijini Lagos. Majizzo alimsindikiza muigizaji huyo ambaye jina lake halisi ni Elizabeth Michael na akawa bahati kwake kwasababu alishinda.
Baada ya hapo tetesi za uhusiano wao zikawa kubwa zaidi. Uhusiano wao sasa unaonekana kuwa wazi zaidi licha ya kuzungukwa na maneno ya hapa na pale hasa kutokana na Majizzo kuachana na mzazi mwenzake, Hamisa Mobetto. Warembo hao kwa sasa ni kama paka na panya na timu zao zimewahi kurushiana vijembe mtandaoni.
Bado hata hivyo Majizzo na Lulu hawajataka kuyaweka wazi mambo ya faragha mara kwa mara na hivyo kuwafanya wengi kutaka kuwachimba zaidi.
Umaarufu na ushawishi wa Lulu ukiunganishwa na sifa za ujasiriamali na utajiri alionao Majizzo (Dj maarufu aliyewika zamani) kwakuwa Mkurugenzi Mtendaji wa EFM unaifanya couple hii iwe na nguvu sana.

8. Harmonize na Jacqueline Wolper

e0ca9c67-c1e2-49d5-8fad-aef387a7d3b9
Harmonize ametoka kwenye maisha duni ya kulala stendi ya mabasi hadi kusaini label inayomilikiwa na msanii mkubwa Afrika. Hiyo haikutosha, alienda mbali zaidi kwa kuanzisha uhusiano na mmoja wa mastaa wakubwa wa filamu nchini na gwiji wa fashion, Jacqueline Wolper.
Hadithi ya uhusiano wao inavutia pia. Wolper aliwahi kuwa na uhusiano na Diamond ambaye leo hii wamebaki wakiitana ‘mkwe’ huku Harmonize akipewa baraka za kufaidi kilichowahi kuwa mali ya bosi wake. Uhusiano wao uliteka vichwa vya habari ndani ya muda mfupi. Wengi walidhani ni kiki lakini baada ya muda mfupi kila mmoja alishangaa jinsi walivyozama kwenye mahaba mazito.

9. Quick Rocka na Kajala

Kajala-na-Quick
Nimeanza kuusikia uhusiano wa Quick Rocka na Kajala muda mrefu sana. Wao pia hawakuwa tayari kuuweka wazi na waliendelea kukanusha kuwa pamoja kwa kipindi kirefu. Lakini kama wasemavyo kuwa penzi ni kikohozi kulificha huwezi uhusiano wao ulithibitishwa katika mazingira tofauti tofauti ikiwemo video aliyopost Quick akimbusu muigizaji huyo.
10. Nahreel na Aika
12543287_1125680584111594_2090272718_n
Nahreel na Aika wametoka mbali. Kutoka kusoma pamoja India wakiwa na kundi la Pah One, hadi kutengeneza si tu kundi maarufu Afrika Mashariki, Navy Kenzo bali pia kuanzisha studio na label yao, The Industry. Kwa wanaowafahamu, watakubaliana nami kuwa, Nahreel na Aika si tu wapenzi, bali pia ni mtu na mshkaji wake na partiners kibiashara wanaoelewana kinoma.

CHECK OUT VIDEO MPYA YA G NAKO FT NIKKI WA PILI - LAINI

Rapper wa kundi la Weusi G Nako ameachia video mpya ya wimbo “Laini”, akiwa amemshirikisha Nikki wa Pili. Video imeongozwa na Freeman Richard.

MRITHI WA NAY WA MITEGO KWA SHAMSA FORD ANAKULA BATA BALAA *PICHAZ*

mmk
KIKOHOZI cha mapenzi kinaendelea kumkaba malkia wa filamu Shamsa Ford. Baada ya kupigana chini na rapper Nay wa Mitego na kuapa kutomwanika tena mpenzi wake mpya katika mitandao ya kijamii, Jumamosi hii hali imemshinda na kuanza kushare picha mbalimbali akiwa na mtu wake wa karibu.

Muigizaji huyo mahiri wa filamu ambaye ni mama wa mtoto mmoja, miezi michache iliyopita baada ya kuachana na Nay wa Mitego, aliaambia Bongo5 kuwa hatarudia tena kushare picha za mpenzi wake katika mitandao ya kijamii.
Mrembo huyo Jumamosi hii ameshare picha mbalimbali katika mtandao wa kijamii akiwa na mtu wake wa karibu na kuandika ujumbe huu:
Kuna muda unaweza ukafanya kitu mtu akakuona mshamba au limbukeni. Ila ukweli ni kwamba hakuna mtu anaweza jua hisia za mwenzie anavyojisikia kwa wakati ule zaidi ya yeye mwenyewe. .TUHESHIMU HISIA ZA WENZETU. …I love you a man of my dream…NICE Saturday
4K0A7304
mm
Baada ya kupost ujumbe huyo, mashabiki wake katika mitandao ya kijamii wamekuwa na maoni haya.
Winfridajames120
Dashamsa mbona una mficha shemeji ukiibiwa utaanzakulala mika Oooh nimeibiwa na wakati utaki kumtambulisha watu wamjue mapema
Halimarashidimbwed
Ila huyu ni Ney bhana.. Hhhh ila kama ni Ney kweli umempenda simalizii maneno mpaka ni prove ndiye…. Nitatomboka siku hiyo ila yenye heri tu kwani kuna picha nimelisoma nitalidadavua @shamsaford

iam_innocentshayo
Yaaa inajua ifike muda mjue kuwa naye pia ni mwanadamu,, anapenda awe na mtu anayempenda na kumjali,,, ni ngumu kusema asipendwe au asiwe na mpenz kisa nyie mashabiki au jamiii,, basi muacheni afanye yampasayo mwanadamu kufanya yeye si robot,, kama akiwa na wanaume wengi ni yeye,, kama akiwa uchi ni yeye,, maana ndo ilipo furaha yake,, muacheni afurahi msimhukumu maana hamna malaika hapa duniani

betywaukweli
Hv mnataka aishi bila mwanaume?nyie hamna wenu?au kwakuwa yeye star?nyie kubadili kila cku na c kubali kuwa wazi mnao rundo .kila mtu na yake.mlitaka avae mashungi kwani kazoea?clna hapo uchi uko wp au kisa kalala na huyo?sh jmn mlitaka alale na ushungi?

''MAFANIKIO YA MSANII NI KIPAJI CHAKE KUSAIDIA JAMII'' - PROF. JAY

Professo-Jay
MBUNGE wa Mikumi na msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop Bongo, Joseph Haule maarufu kama Professor Jay amesema mafanikio kwa msanii siyo kumiliki mali nyingi bali ni jamii kuweza kunufaika kutokana na kipaji chake.
Akiongea na Dj Niko Track kwenye kipindi cha Dj Show cha Radio One, Professor Jay alisema kuwa mafanikio ni kitu kile kinachoonekana na kuleta tija na maendeleao kwa watu, lakini pia yanaweza kugawanyika kwa watu wengine siyo ya kwako peke yako.
“Wasanii waliofanikiwa majina yao yanaweza yakatumika kama alama ili kuinufaisha jamii. Wasanii kama Lady Jaydee, Professor, Juma Nature ni wasanii ambao kwa talent zao walizokuwa nazo zimekuwa manufaa kwa wengine. Kama Lady Jaydee amekuwa icon kwa wakina mama ambao wamekuwa strong kuweza kusimama pale. Mafanikio siyo kuwa na nyumba wala gari hapana, talent yangu imesaidia nini jamii yangu,” alisema Professor.
Kama Professa unakuta ana ‘Professor Foundation’ ambayo inasaidia hata wasiokuwa wanamuziki wananufaika kwa kidogo ninachokirudisha kwenye jamii. Wale wote wenye mafanikio ni wale wanaoweza kushare na kuruidisha kidogo walichokuwa nacho kwenye jamii,” aliongeza.

ZILIZOSOMWA ZAIDI