MAAFISA wa Secret Service walilazimika kumuondoa haraka jukwaani mgombea wa Urais wa Marekani wa chama cha Republican, Donald Trump Jumamosi hii wakati akiongea kwenye mkutano wa kampeni huko Reno, Nevada baada ya kumgundua mtu aliyekuwa miongoni mwa waliohudhuria kuwa anaweza kuwa hatari kwake.
‘Go! Go!’ maafisa hao walipiga kelele wakati wakimtoa Trump kwenye mkutano huo huku maafisa wa polisi wakimkamata Austyn Crites, 33 aliyekuwa mbele ya umati huo.
Crites anajitambulisha kama mfuasi wa Republican lakini anayemuunga mkono Hillary Clinton, kwa mujibu wa maelezo kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Watu waliodhuhuria wameiambia CNN kuwa walimskia mtu akipiga kelele kuwa kuna mtu ana bunduki. Hakuna kesi iliyofunguliwa dhidi ya Crites.Alipoachiwa na polisi, Crites amesema timbwili hilo lilianza baada ya kuonesha bango lililoandika Republicans Against Trump.
0 comments:
Post a Comment