KLABU ya Manchester United ya Uingereza inaongoza orodha ya vilabu vya soka vinavyolipa mishahara mikubwa duniani.
Kwa mujibu wa The global sports salary survey (GSSS), United imekuwa ikitumia kiasi cha wastani wa paundi milioni 5.77 kumlipa kila mchezaji kwa mwaka.
Timu ya Barcelona ya Hispania inashika nafasi ya pili ikiwa inatumia kiasi cha wastani wa paundi milioni 5.65 kumlipa kila mchezaji wake kwa mwaka.
Wakati huo huo ligi ya Uingereza imedaiwa kuwa ndio inaogoza kulipa fedha nyingi zaidi kwa ajili ya mishahara kwa wachezaji wake ikitumia kiasi cha wastani wa paundi milioni 2,438,275 kwa wiki.
0 comments:
Post a Comment