MCHEZAJI wa Uingereza Joey Barton ambaye haishiwi visa amefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na klaby yake ya Rangers, inayoshiriki ligi kuu ya nchini Scotland.
Barton mwenye miaka 34, mkataba wake ulikua unamalizika mwaka 2018, na ameichezea Rangers michezo nane toka ajiunge na timu hiyo akitokea klabu ya Burnley, mwezi Mei mwaka huu.
Mchezaji huyu alifungiwa muda wa wiki sita na timu yake baada kutokea mabishano katika mazoezi mwezi Septemba, pia amekua matatani kufuatia tuhuma za kukiuka sheria na uchezaji Kamari, na anachunguzwa na chama cha soka cha Scotland.
Zamani alisha wahi kuvichezea vilabu vya Manchester City, Newcastle, Marseille na QPR, amewashukuru mashabiki wa Ranger, na kuitakia timu hiyo mafanikio.
Huu ni ujumbe wa Joey Barton katika ukurasa wake wa mtandao wa Twitter
0 comments:
Post a Comment