ALI KIBA amesema tatizo lililopo kwenye muziki wa Tanzania, ni baadhi ya nyimbo nzuri kutopewa nafasi ya kusikika kama zinavyostahili.
Ametoa kauli hiyo wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Daladala Beat cha Magic FM wakati alipokuwa kwenye ziara ya kupromote wimbo wake na Ommy Dimpoz, Kajiandae.
Ametoa kauli hiyo wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Daladala Beat cha Magic FM wakati alipokuwa kwenye ziara ya kupromote wimbo wake na Ommy Dimpoz, Kajiandae.
“Kuna watu wanaweza wakawa wanajua kabisa huu ni muziki mzuri, kuna watu hawatotaka ukae kwa muda mrefu, hii inatucost sana,” alisema.
“Kuna muziki mzuri, wasanii wanaimba nyimbo nzuri lakini kuna watu wengine hawataki hii haifai hatuwezi kuendelea,” alisisitiza. “Hili suala siwezi kulinyamazia kimya.”
Hata hivyo Ali hakuweza kutolea zaidi ufafanuzi wa kauli yake.
0 comments:
Post a Comment