Saturday, November 21, 2015

WAZIRI MKUU MPYA KASSIM MAJALIWA KASSIM ALIVYOAPISHWA IKULU YA CHAMWINO DODOMA *PICHAZ*

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kassim Majaliwa Kassim kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika hivi karibuni, hafla ya kiapo ilifanyika Ikulu ya Chamwino Mkoa wa Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akimkabidhi hati ya kiapo Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim  baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika hivi karibuni, hafla ya kiapo ilifanyika Ikulu ya Chamwino Mkoa wa Dodoma.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim baada ya kuapishwa  rasmi kushika wadhifa wake huo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma.
 Makamo wa Pili wa Rais wa  Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  akisalimiana na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim baada ya kuapishwa  rasmi kushika wadhifa wake huo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma.
 Makamo wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim baada ya kuapishwa  rasmi kushika wadhifa wake huo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma.
 Viongozi wa Wakuu wa majeshi ya  Ulinzi pamoja na Viongozi mbali mbali waalikwa wakiwa katika hafla ya kuapishwa Waziri Mkuu Mpya wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makamo wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (kushoto) na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim (kulia) baada ya kuapishwa  rasmi kushika wadhifa wake huo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma,
 Watoto wa Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim wakimshuhudia  Baba yao akiapishwa na  leo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli (katikati)akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim (watatu kushoto mstari wa nyuma) baada ya kuapishwa rasmi leo katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wabunge mbali mbali leo wakati waliposherehekea kwa kuapishwa Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim   na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma.
#Picha na Ikulu.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI